April 10, 2016



Leicester imeitungua Sunderland kwa mabao 2-0, yote mawili yakiwa yamefungwa na mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy.

Vardy amefikisha mabao 21 akiwa anakimbilia ufungaji bora, huku Leicester iliyobakiza mechi tano tu za Ligi Kuu England ikiwa imeanza kusikia harufu ya ubingwa.

Ushindi huo unaifanya ifikishe pointi 72, nafasi ya pili Tottenham wakiwa na pointi 62 na Arsenal katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 59.















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic