May 29, 2016



Yannick Ferreira Carrasco ni raia wa Ubelgiji, ana miaka 22 tu, ndiye alifunga bao la Atletico Madrid katika dakika za mwisho na kuikoa na kipigo cha ndani ya dakika 90 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Carrasso ambaye mzazi wake mmoja ni Mbelgiji na mmoja ni Mhispania ni kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji pia ni kati ya wachezaji vijana waliopita hatua zote kwa ubora wa juu.

Moja ya timu alizopitia ni Genk ambayo sasa anaichezea mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta, baada ya hapo akapelekwa Monaco B ya Ufaransa katika kupandishwa katika timu ya wakubwa ya Monaco 2012 hadi 2015 yaani mwaka jana alipojiunga na Atletico Madrid.


Ameichezea Atletico Madrid mechi 29 akiwa amefunga mabao 5 kabla ya Kocha Diego Simeone kumuamini leo na kumpa nafasi ya kucheza katika mechi hiyo kubwa kuliko zote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Anaaminika kuwa mmoja wa viungo washambuliaji wenye uwezo wa juu kabisa katika bara la Ulaya baada ya miaka miwili au mitatu ijayo kama ataendelea kudumisha kiwango chake.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic