May 27, 2016


Sasa lile tamasha pendwa la Majimaji Selebuka 2016 lililosubiriwa muda mrefu limetimia ambapo kesho Jumamosi kutashuhudiwa mchezo wa riadha ukikata utepe kwa mbio ndefu na fupi.

Tamasha hilo linaloratibiwa na Asasi ya Somi, lenye lengo la kuinua vipaji vya michezo nchini pamoja na kumuinua mwananchi kupitia elimu ya ujasiriamali, linafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini Songea na litadumu kwa wiki nzima hadi Juni 4, mwaka huu.

Tamasha litafunguliwa saa 12 asubuhi kwa mbio fupi za Km 5 kisha mbio ndefu za Km 42, 21 na 10 kisha fupi za Km 5.
Mratibu wa tamasha hilo, Reinafrida Rwezaura amesema mbali na riadha pia ni siku ya ufunguzi wa maonyesho ya ujariamali  ambayo yatadumu mpaka Juni 3, mwaka huu.

“Kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi watatu kama medali, ngao, vikombe, fedha taslim pamoja na zawadi ndogondogo kutoka kwa wadhamani kwa shughuli/mchezo husika,” alisema Reinafrida.

Kesho Jumapili ni mashindano ya ngoma za asali pamoja na utalii wa ndani katika Mbuga ya Wanyama ya Luhira. Shughuli nyingine ni mdahalo kwa shule za sekondari, utalii kwa vivutio vingine kama Mbamba Bay, Mbuga ya Matogoro na Kingole na litatamatishwa na mchuano mkali wa mbio za baiskeli Juni 3, mwaka huu ambapo ukiachilia mbali zawadi watakazopata, pia wanawania fursa ya kwenda Rwanda kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo kwa siku 10.

Bado hujachelewa na unaweza kujisajili kushiriki kuwania zawadi mbalimbali katika michezo iliyobaki huku kwa upande wa riadha mwisho wa usajili ni leo kabla ya saa 12 asubuhi.


Fomu zinatapatikana kwenye Ofisi ya Maleta Ndumbaro Tawi la Songea, Heritage Cottage Hotel, Mama D Café, Makumbusho (zote Songea) na Tovuti ya www.somi.international kwa gharama ya 10,000 na kwa Kikundi cha ujasiriamali ni 50,000 lakini mjasiriamali mmojammoja ni 10,000.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic