May 4, 2016



Nahodha wa Simba, Mussa Mgosi amekiri kuwa sababu kubwa ya kushindwa kuifunga Azam FC na kuishia kutoka sare ya bila kufungana ni wao kucheza chini ya kiwango. 
Mgosi alienda mbali kwa kusema; “Hatukuwa makini katika kipindi cha kwanza kwani tulipata nafasi nyingi za kufunga lakini hatukuzitumia.”

Matokeo hayo yaliifanya Simba kufikisha pointi 58 nyuma ya Azam yenye pointi 59 huku Yanga ikiongoza Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 65. 

Mgosi alisema, Simba ilicheza kwa kiwango cha chini hasa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kwani wachezaji hawakuwa wamechangamka hivyo kushindwa kufunga.

“Kipindi cha pili baada ya maelekezo mambo yalibadilika ndiyo maana kidogo uhai ulionekana. Kutokana na hali hiyo, sasa hakuna matumaini tena ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.


“Ila kama tungeifunga Azam na kufikisha pointi 60, tungekuwa na nguvu ya kupambana ili kutwaa ubingwa lakini kwa sasa Yanga ndiyo ina nafasi zaidi ya kutwaa ubingwa,” alisema Mgosi.

Mgosi ndiye mchezaji mkongwe zaidi kati ya walioichezea Simba msimu huu.

1 COMMENTS:

  1. Simba kila siku "tutajipanga"tutajipanga,sasa yapata miaka 3.Nyie hamjui tu,kuna laana inawatafuna na msipoangalia na mwakani mtaishia kujipanga tu.Ngojeni kuona na kuwashangilia waarabu wakija kucheza na wakimataifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic