May 6, 2016



Na Saleh Ally
LIGI Kuu Bara inakwenda ukingoni, mabingwa watetezi Yanga, wanaonekana wana nafasi kubwa zaidi ya kuwa mabingwa kwa mara nyingine.

Yanga wana pointi 68 wakiwa kileleni, wanafuatiwa na Azam FC wenye 59 na Simba 58 huku kila timu kati ya hizo tatu ikiwa imebaki na mechi tatu mkononi.

Mwendo ulivyo, mambo yamebadilika kabisa. Awali Simba alionekana ni mshindani mkubwa wa Yanga na Azam FC, lakini sasa inaonekana Azam FC tena kidogo inaweza kushindana na Yanga.

Ukiachana na mbio za vigogo hao kileleni. Angalia hali hiyo namna ambavyo washambuliaji wa kigeni wanavyozidi kupasua anga kuwania nafasi ya kiatu cha ufungaji bora katika ligi hiyo.

Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe tayari ana mabao 20, akiwa ameweka rekodi mpya. Awali hakuwa amewahi kufunga idadi hiyo na kipindi kimepita tokea mshambuliaji kufunga idadi hiyo.

Anafuatiwa na Hamisi Kiiza kutoka Uganda mwenye 19. Hawa wawili walikuwa gumzo kubwa mwezi mmoja uliopita kutokana na namna walivyokuwa wakikimbizana, japokuwa sasa Mrundi huyo amekaa kileleni.


Yako mengi unaweza kuyazungumza kupitia Ligi Kuu Bara namna inavyokwenda na kasi yake. Nani anaweza kuwa bingwa, nani anaweza kuwa mfungaji bora. Wachache sana wanaokumbuka hilo kwa kuwa gumzo kubwa ni kuhusiana na rushwa katika soka.

Viongozi mbalimbali wanalumbana kuhusiana na suala la rushwa. Wako wanaotuhumu upande mmoja wakitoa maelezo namna rushwa inavyotumika kusaidia bingwa kupatikana.

Wako wanaozungumza na kuwataja wengine, wako walio tayari kuwafikisha wengine kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakiona wametajwa au vinginevyo.

Kwa kifupi hakuna anayeweza kukataa kwamba katika kipindi hiki, gumzo katika mpira wa Tanzania ni suala la rushwa ambalo ni adui mkubwa wa maendeleo.

Tunajua kuna sakata la upangaji matokeo na tayari TFF imewafungia watu hadi miaka 10 na faini kubwa za hadi Sh milioni 10. Siku chache baadaye, viongozi wa juu wa shirikisho hilo, wakaingia matatizoni baada ya sauti zao kusikika wakipanga matokeo. Sasa tuhuma hizo zinafanyiwa kazi ili kupatikana kwa jibu sahihi.

Wakati suala la TFF bado halijatulia, saa hizi, gumzo ni rushwa ya ligi kuu ndiyo linachukua nafasi kubwa na hata viongozi wa timu mbalimbali nao wamekuwa wakilizungumzia!

Nani anaweza kusema tena hakuna rushwa katika soka ya Tanzania? Nani ana uwezo wa kukanusha hilo na kuweka msisitizo kwamba suala hilo ni rushwa na ndiyo maana limekuwa likifichika?

Kwa matatizo yanayotokea na gumzo lililopo sasa, si siri tena kwamba rushwa ipo ndani ya mpira wa Tanzania na inatambaa kwa kasi kubwa. Huenda baada ya kipindi fulani itaudumaza kabisa mpira wenyewe uwe hauwezi hata kufumbua macho.

Kama mpira wenyewe unakwenda mwendo wa kutambaa leo zaidi ya miaka 30. Vipi adui rushwa kama ataingia ndani ya macho ya soka na kufanya kinachotokea sasa.

Hakuna ubishi tena, lazima tukubali kama rushwa ipo ndani ya soka ya Tanzania. Basi wahusika wakuu ni wadau wa soka yenyewe ambao ni viongozi, waamuzi, wachezaji na wengine, jambo ambalo si sawa.

Kuzungumzia rushwa katika mpira wa Tanzania ni kuwagusa watu wengi sana. Wakiwemo vigogo na wale wa kati na chini wanaofaidika na hilo na huenda inaweza kuwa rahisi sana kujitengenezea uadui kwa kuwa hawatafurahia kuona unawaharibia duka lao ambalo linawafaidisha kimaisha tena kwa njia ya mkato.

Ukweli ni hivi; lazima tuseme bila ya kujali nani atakasirika na kujenga uadui. Kwani ili mpira uendelee lazima uwe kwa ajili ya wengi, yaani Watanzania. Kama utaendelea kuwa kwa manufaa ya wachache, basi hata maendeleo yatakuwa kwa faida yao na matumbo yao ambalo si jambo sahihi.

Pazeni sauti zenu, pigeni kelele na kukataa hili suala la rushwa. Wako wanaotaka kulificha au kulisaidia ili liendelee nao kufaidika. 

Kuendelea kwao ni kuutafuna mpira wa Tanzania ambao tunaulilia kila kukicha lakini hauna mabadiliko hata kidogo na ndiyo maana utamu wa gumzo la kisoka, umehamia kwenye utamu wa rushwa inavyoweza kutembezwa.


4 COMMENTS:

  1. Kwa nini usifanye investigative journalism unaishia kubwabwaja kama mtu wa mtaani? Kunaweza kuwa na tatizo mahali na wala halijaanza leo katika soka la Tanzania. Jitoe kimasomaso fanya utafiti kisiri uje na vitu vya uhakika. Hakika jamii ya wapenda soka itashukuru.
    Haisaidii kuandika kama watu wa viweni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Rushwa ipo hata kwa washika kalamu(waandishi wa habari) ndio maana utaona habari za kuchafuana zinatawala sana kuliko za kuendeleza kabumbu.Inawezekana hata huyu aliyeleta mada hii naye ni muhathirika wa rushwa kwa aina moja au nyingine kwani tukumbuke jinsi alivyokuwa akimpigania AVEVA kuingia madarakani huku akimwandika vibaya Wambura.Sisi tusubiri kushangilia wenzetu wa Ulaya tuu hapa michosho kwa laki mbilimbili!

      Delete
    2. Huyu mwandishi nimeanza kustukia makala zake. Uongo mwingi sana. Nilifuatilia sana alivyomshupalia Rage kuwa kala hela za uhamisho wa Okwi. Baadaye tumeona yalikuwa maneno ya vijiweni au alikuwa anatumiwa na maadui wa Rage pole Simba.

      Delete
    3. Huyu hana jipya mbna kila SKU watu wanampondea abadilike tu saleh jembe jipu kila kitu kikimuuma anakutaftia sababu huu unazi kwa waandishi sio mzur tumien kalamu yenu vizur msiwe chachu ya uchochez kwa uandishi wa ushabiki

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic