May 15, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
-KADI Ally Shariff wa Mtibwa analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Kazimoto anaingia vizuri kabisa lakini anashindwa kutoa krosi nzuri
KADI Dk 85, Kazimoto analambwa kadi ya njano kwa utovu wa nidhamu
SUB Dk 80, Mtibwa wanamuingiza Ally Yusuf kuchukua nafasi ya Javu
Dk 78, Mtibwa wanapoteza nafasi nyingine nzuri, Muzamilu anapaisha wakati angeweza kumpa mpira huo Javu
Dk 72, Mpira wa kwanza, Gole akiwa na kipa Manyika anapaisha juuu
Dk 71, Maulid Gole anaingia kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya
GOOOOOOO Dk 70, krosi safi ya Tshabalala anapiga krosi safi na Banda anaruka na kupigwa kichwa safi sana, baooo la Simba

Dk 66, Mgosi tena anapata nafasi nzuri baada ya kona ya Isihaka, anabutua puuuu
DK 60 hadi 63 bado mpira unaonekana kuchezwa katikati zaidi na kila wanapokaribia langoni wanabutua bila utulivu
Dk 57, beki Dickson Daud anawachambua mabeki watatu wa Simba, lakini akiwa karibu na lango kabisa anashindwa kufunga baada ya kuukosa mpira

SUB Dk 55, Mtibwa wanamtoa Bahanuzi aliyeumia nafasi yake inachukuliwa na Vicent Barnabas
Dk 47, Lufunga anazubaa, Bahanuzi anaachia bunduki kali hapa lakini mpira unapaa juuu
Dk 46, Simba ndiyo wanaoanza kwa kasi, shambulizi la kwanza, krosi nzuri ya Tshabalala lakini Vicent tena anaiwahi na kuokoa

MAPUMZIKO
-Mwalyanzi anapiga vizuri mpira wa adhabu, Said Mohammed Nduda anapangua na kuwa kona, inachongwa na anadaka vizuri kabisa Nduda
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 42 na 45, Simba wanaendelea kupoteza nafasi za kufunga na kuonyesha hawako makini katika umaliziaji
Dk 41, krosi nzuri, Mgosi akiwa hatua tatu nje ya lango la Mtibwa anapiga kichwa kinapaa juuuu kabisa
Dk 37, Beki Vicdent Andrew anaokoa mpira uliokuw aunakwnda kuvuka mstari wa lango
Dk 30, Javu anapiga krosi nyingine matata kabisa, hatariiii, Simba wanaokoa
Dk 28 Mtibwa Sugar wanapoteza nafasi ya wazi kabisa baada ya Muzamilu akiwa hatua tano kutoka langoni anashindwa kufunga
Dk 26, Mgosi anamtoka Vicent kwa kasi kabisa, lakini Dickson Daud anawahi na kuutoa
Dk 18 hadi 21, mpira unaonekana kuwa wa kasi lakini bado hakuna timu inayoonekana kuwa makini kwenye lango la mwenzake

Dk 16, Ndemla anabutua shuti kuuubwaaa bila sababu, goal kick
Dk 14, Simba wanapoteza nafasi nyingine nzuri baada ya krosi safi ya Tshabalala kutua katikati ya lango lakini wanashindwa kuunganisha
Dk 11, Simba wanapata nafasi nzuri kabisa, Mgosi anapiga krosi lakini Mwalyanzi anashindwa
Dk 4 hadi 7, kidogo Mtibwa wanaonekana kucheza vizuri lakini taizo kubwa kumalizia
Dk 2, Mgosi anapiga kichwa kinagonga mwamba na kurudi uwanjani
Dk 1, Simba inaanza kwa kasi ikipeleka mashambulizi ya haraka


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic