May 2, 2016



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.

Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.

Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.

Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kadhalika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea  kesho Mei 3, 2016 kwa mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.


Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic