May 11, 2016

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ameipongeza timu ya soka ya Young Africans ‘Yanga’ kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.

Hii ni mara ya 26 kwa Yanga ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.


     


    “Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.

Kadhalika Rais Malinzi amezikumbusha na kuhamamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kutoa maoni, mapendekezo, marekebisho ya ili kuboresha kanuni za uendeshaji wa ligi hiyo kwa msimu ujao. Maoni hayo yapelekwe kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com

Yanga imefikia rekodi hiyo baada ya kutwaa ubingwa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006 na misimu ya 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013, 2014-15 na 2015-16.
Pamoja na kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2015/2016, kikosi cha timu ya Young Africans kwa sasa kimebakiza michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ndanda unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Mei 14, 2016 kadhalika dhidi ya Majimaji Mei 22 ambayo itakuwa ni siku ya kufunga pazia la Ligi Kuu msimu huu wa 2015/16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic