May 3, 2016

MPIRA UMEMALIZIKA: FULL TIME

STAND UNITED 1-3 YANGA 

Dakika ya 90+3: Muda wowote mchezo utamalizika.

Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 86: Mchezo unaendelea kwa kasi.

Tambwe anacheza faulo, anapata kadi ya njano.

Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Salum Telela ameingia Mbuyu Twite.

Dakika ya 82: Maguri anapiga penalti na kufunga, Stand wanapata bao moja

MAGURIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Kamusoko alimchezea faulo, Seleman Kassim wa Stand mwamuzi akaweka penalti.

Dakika ya 81: Stand wanapata penalti.

Dakika ya 69:Kamusoko anapiga shuti kali lakini linatoka hatua chache kutoka langoni.
 
Dakika ya 75: Yanga wanafanya mabadiliko, Ngoma anatoka anaingia Matheo.

Dakika ya 70: Stand waapata kona, wanapiga lakini inatoka nje.

Mashabiki wa Yanga wameanza kupagawa kwa mabao matatu mpaka sasa.


Dakika ya 63: Tambwe anafunga bao kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Simon Msuva.

TAMBWEEEEEEEEEEEEE

Dakika ya 60: Maguri anakimbia na mpira pembeni ya uwanja, anaingia katikati ya uwanja lakini juhudu zake zinashindwa kuwa nafaida baada ya Yanga kuondoa hatari. 

Dakika ya 58: Mchezo bado haina kasi sana ila Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 52: Msuva anakosa nafasi ya wazi.

Dakika ya 49: Watu wa usalama wanaenda upande ambapo mashabiki wanafanya vurugu, wanawatuliza na mchezo unaendelea.

Dakika ya 48: Mchezo umesimama kwa muda kutokana na baadhi ya mashabiki kumfanyia fujo mwamuzi wa pembeni.
 
Dakika ya 46: Mchezo umeanza

Kipindi cha kwanza kimekamilika, Yanga inaongoza mabao 2-0.
 
Zimeongezwa dakika mbili

Dakika ya 45: Ngoma anafunga bao la pili baada ya kupitishiwa pasi nzuri kutoka katikati ya uwanja huku walinzi wa Stand wakijua ameotea.

Dakika ya 38: Mchezo umesimama, Ngoma anatibiwa.

Dakika ya 37: Ngoma yupo chini ameumia lakini mchezo unaendelea.

Dakika ya 35: Yanga wanafanya shambulizi lakini kipa wa Stand anaokoa. 

Dakika ya 30: Yanga wameanza kumiliki mpira muda mwingi
KOCHA WA STAND UNITED, LIEWIG


Dakika ya 24: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 20: Stand wanamiliki mpira muda mwingi sasa.

Dakika ya 17: Elius Maguri anapiga shuti lakini linakuwa mchekea kwa kipa wa Yanga.

Dakika ya 11: Yanga bado inaongoza bao 1-0, mchezo bado haina kasi licha ya Yanga kufunga bao la mapema.

Stand walipanda kufanya mashambulizi , Salum Telela wa Yanga akaunasa mpira akapiga ndefu, mshambuliaji wa Yanga, Donlad Ngoma akaunasa akakimbia nao na kwenda kufunga.

 

Dakika ya 2: Ngoma GOOOOOOO!!!!

Dakika ya 1: Yanga wanafanya mashambulizi.

Mchezo umeanza
  
Timu zimeshaingia uwanjani, sasa ndiyo zinakaguliwa.

2 COMMENTS:

  1. Thats the mentality of champions, they have to distinguish themselves from others... Bravo DYA (dar young africans) one step ahead. Be prepared for the Angolans....

    ReplyDelete
  2. Oooh wanabebwa!!!! Mara wale viporo kwanza!!!! Kiporo anavimbiwa mzungu, ila mbongo ni jadi yetu... ! Msimbazi wana matokeo ya kambarage stadium kweli???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic