May 17, 2016


Uandishi ni kazi inayotaka watu wanaofuata weledi, watu wanaoamini kwenye ukweli na wenye ndoto hasa ya kufanikiwa kwa maana ya kuifanya kiufasaha.

Siku hizi mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa, kila siku zinavyosonga, waandishi wenye ndoto ya kuwa maarufu huku uwezo wa wa utendaji ukiwa chini na duni, wanazidi kuongezeka.

Waandishi wanaoamini wanajua sana, wasiotaka kuambiwa, wanaomini wanajulikana, wameongezeka.

Juzi niliona picha za waandishi watatu, wawili wakiwa wamevaa medali za ubingwa wa Yanga, mmoja akiwa amebeba kombe tena akiwa anafurahi kwelikweli, jambo ambalo sijaliona katika miaka yangu 18 ya uandishi wa habari wa ushindani.

Nilishangazwa sana, ajabu kila mmoja wapo alionekana kitu cha kawaida bila ya kukumbuka si sahihi kiweledi, ajabu hakuna aliyekumbuka kufanya hivyo ni kuvidhalilisha hata vyombo vya habari wanavyofanyia kazi.

Nilielezwa wanatokea Dimba, Lete Raha na Majira. Nikaamua kuzichukua picha hizo na kuzitupia kwenye blog hii ili watu waone vituko hivyo. Lengo langu nilitaka watu waone, pia sikuona ajabu kwa kuwa wao wenyewe tayari walitupia mitandaoni, sehemu watu mbalimbali wanaweza kuwaona bila ya kificho, haikuwa siri tena.

Kwa kuwa sina bahati au muda ya kuingia kwenye kurasa zao za Facebook, sikubahatika kusoma wakiandika matusi ya ajabu kabisa unayoweza kuyalinganisha na watu wanaojipanga mitaani kuuza miili yao wanapokuwa wanagombana na wateja wao. Sijawahi kutishwa na matusi, sijawahi kuangushwa na matusi, sijawahi kuumizwa na na wenye akili ndogo.

Ajabu, Kamwe naye aliona hilo ni sahihi. Akasema maneno mengi huku akiwataja hadi wazazi wangu, kabisa kama ilivyo kwa mwanadada anayetokea Lete Raha ambaye nilielezwa jina lake halisi ni Devotha Kihwelo ambaye amejipachika jina la ‘kistaa’ Devjay.

Hapo ndipo nilipoanza kugundua fani inakwenda mlama, kwanza Kamwe akaweka picha akiwa na kwenye runinga akishangilia ubingwa wa Leicester kutaka kuonyesha si ajabu kwa kuwa alishangilia kombe la Leicester ambalo alilishika kwa hisia kupitia runinga!

Nikashangazwa zaidi, huenda picha ya muonekano wa nje inaweza ikawa haifanani na injini iliyo ndani ya mwili wa mtu husika. Hajui tofauti ya Yanga na Leicester? Hajui hasara kwa mwandishi kujiingiza kwenye ushabiki tena hadharani? Hajui watu wanaweza vipi kumpuuzia kusoma anachoandika (ambacho sijawahi kusoma hata mara moja), kutokana na kuonyesha ushabiki mandazi kama ule!

Najua aina yake, uwezo wake, lakini sikuweza kuupima kufikia kiwango duni kiasi hicho. Kwamba ni mwandishi anayeweza kushindwa kujibu hoja na kuvurumisha matusi kama ambavyo majuha wanavyoweza kulumbana bila kuangalia msingi sahihi wa kinachozungumzwa.

Kweli huyu dogo ambaye kama uzoefu ungehesabiwa kwa Krismasi, hana hata Krismasi nne kwenye uandishi. Vipi asijue ujinga aliofanya kuhusu kuonyesha yeye anafurahia kombe, lakini ajabu bado hajui kuwa ndiye alikuwa wa kwanza kujianika kwa kuweka picha mtandaoni. Au hajui mtandao wa Facebook ni wa kijamii na ukiweka picha tayari inaweza kuwa habari?

Nikawaza, watu wa namna hii wanatengenezwa wapi? Kweli anaamini yeye ni mwandishi, asiye na uwezo wa kujibu hoja anavurumisha matusi ya nguoni. Nani aliye imara anaweza kutishwa na matusi au kashfa za kulazimisha?

Nikasema hivi; nitaanza taratibu hivi, baadaye nitapandisha sauti tu. Acha tuanze na sauti ya muziki unaopigwa nyumbani, baadaye tutafikia ule unaopigwa kwenye kumbi za muziki, huenda itakuwa rahisi kusikika kwa watu wenye masikio mabovu na pua zisizonusa kwa kuwa macho yao hayaoni mbali.

Wakati namshangaa kaka, dada naye alionekana ni kichwa maji maradufu. Maana alichukua picha yangu nikiwa na Elizabeth Michael ‘Lulu’ pamoja na Monalisa tukiwa na furaha baada ya Lulu kushinda tuzo Nigeria. Nilisafiri hadi Nigeria kwa kazi hiyo, kuripoti Watanzania watatu wakishindana na Wakenya na Waganda. Mungu akasaidia Watanzania wawili wakaipeperusha bendera yetu vizuri na kuwabwaga majirani zetu Wakenya na Wakanga. Huyu dada naye akasafiri hadi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kwenda kuvaa medali! Halafu akafananisha pia, hajui hata Yanga ilikuwa inashindana na kina nani, misingi ya uandishi inasemaje? Pamoja na kwamba hajui, bado hataki kuelezwa...!!!

Baadaye akaweka picha akiwa anashangilia ubingwa wa Thomas Mashali na kubeba ubingwa. Hii alikuwa akifananisha ubingwa wa Yanga alivyovaa medali na ule ubingwa Tanzania Bara waliobeba Yanga!

Huu huenda kwangu ni mshituko mkubwa kabisa, kwamba naye huyu hajui tofauti ya tuzo ya Lulu na ubingwa wa Yanga, au mkanda wa Mashali na ubingwa wa Yanga!


Kama kweli ni mwandishi na hajui hilo, basi ni maajabu. Huwa anaandika nini? Anawaandikia akina nani, masikini wasomaji, wanasomaje na inakuwaje? Ajabu kabisa.

Huyu alijitahidi hata kutukana matusi, (Nikabaki palepale kuwa ukiona mtu anajibu lolote kwa kutukana matusi, jua si mjenga hoja, ana uwezo mdogo wa kufikiri na kuamua, hivyo matusi inakuwa ni defensive mechanism).

Tena akasema, picha yake iliwekwa kwenye blog kwa kuwa hakukuwa na cha kuandika, kwa kuwa yeye ni dada mrembo. (Huenda tunatofautiana utazamaji, unaweza kuangalia mwenye picha na kukubali au kukataa alichosema).

Mwandishi huyo mchanga mwenye umbo la upole na mteremko moja kwa moja kama barabara hafanani na anachozungumza.

Kuna ule msemo: “Hauwezi kupima akili ya mtu kwa kumtazama, vema akazungumza.”

Rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa kashangazwa na ujuha wa vijana hao wanaochipukia kugombea nafasi ya kuwa waandishi hapo baadaye. Lakini akasema niachane nao kwa kuwa ni wajinga, hakuna haja ya kubishana nao.

Msisitizo wangu ukawa hivi: “Haitatokea nikabishana nao, lakini kwa kuwa niko ndani ya fani, tunapambana kupata watu bora, siwezi kuacha wajinga wapite mbele yangu kwa kisingizio eti tutakuwa tunalumbana. Lazima nitawasalimia kwa hatua.”

Fani ya uandishi wa habari inaporomoka kwa sababu ya waandishi wachache wasiojiwelewa au waliingia huku kwa bahati mbaya, kawaida kosa la mtu mmoja, hata kama hana vigezo vya kuwa mwandishi anayejitambua nalo huitwa kama kosa la “Waandishi”. Mwandishi ni binadamu ambaye ana haki ya kushangilia. Lakini ni mtumishi wa umma ambaye anapaswa kuwa kati na kuwa msemakweli.

Kama mtu anavaa medali ya Yanga, kesho anaweza vipi kuwakosoa Simba wakamuelewa. Kwa miaka 18 ndani ya uandishi wa habari, nimezishuhudia Yanga na Simba zikipokezana kombe la ubingwa wa Bara, pia Azam FC. Hawa ambao wanashuhudia mara ya kwanza au ya pili kweli wameshindwa kujizuia?

Mwandishi unavaa medali? Medali ambayo mchezaji kaipigania kwa msimu mzima, inakupa furaha wewe?

Waandishi hawa hawajui kwamba Yanga haiwezi kuchukua ubingwa milele. Siku moja itakuwa Simba, Azam au timu nyingine, watakwenda tena kuvaa medali?

Waandishi hawa hawajui utaifa na mapenzi ya klabu, hawajui tuzo ya Lulu ni utaifa, mkanda wa Mashali ni utaifa. Wanakoandikia wanawaamini vipi? Je, waandishi wa namna hii ni chanzo cha vyombo vya habari au waandishi wa michezo kudharaulika? Wametokea wapi? Na kwanini hawajui wanapokwenda? Malezi mabovu, uwezo mdogo wa kufikiri, malimbukeni au mambumbu?

Ajabu hawataki kuripotiwa na wao ndiyo wameweka picha mtandaoni? Hilo nalo hawajui linavyofanya kazi? (hapa natia tu msisitizo).

Kila mtu anaweza kuwa mwandishi, lakini si lazima wote lazima tuwe waandishi.







11 COMMENTS:

  1. Pole saleh jembe kwa kuumia kisa wenzako wanafurahi hakuna kipengele cha mwandishi wa habari kuzuia furaha ya ubingwa coz hawahusian kwa namna yoyote kuchochea timu Fulani isifanye vizur hivi kwann unapost mbumbumbu kila siku ktk makala zako .....wangekua marefa au watu wa tff ungekua na logic kwa mwandishi wa habar huna logic nenda darasani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma kwa makini alichokiandika Saleh na jitahidi uelewe logic. Acha kukurupuka kaka.

      Na pia inawezekana hufahamu (kama hao wenzako waliovaa medali) kuwa tasnia ya uandishi wa habari ni nyeti kiasi gani. Chukua muda wako tafuta Rwanda na tsnia ya habari utajifunza kwann nasema hivyo.
      Narudia tena acha kukurupuka mjomba.

      Delete
    2. We nae ndio wale wenye uwezo mdogo wa kufikiri... Saleh Ally Kilichompelekea kuandika hvyo ni kwa kuwa hao waandishi ambae ni abdul mkeyenge na wenzake wamekiuka ETHICS za Journalism. Na ndio maana Kwa ku-clarify zaidi saleh ally ameonyesha kuwa alipiga picha na Lulu ni kwa kuwa tu alikua Amewakilisha TAIFA yaani, kwa hapo anakua kama hajaegemea upande wowote.

      Delete
    3. Yawezekana wewe REAL BEDA, ukawa wale wale wanaofikiri kwa kutumia makalio na sidhani kama unajua maana ya 'Ethics', kwa kifupi nikwambie Ethics maana yake ni maadili. Uandishi wa habari una MIIKO na MAADILI yake nadhani hata kwenu kuna miiko na maadili au katika kazi yako kuna vitu kama hivyo lakini kama huelewi kilichozungumziwa ni bora ukakaa kimya kuliko kujipaka mavi ambayo huyo unayemtetea tayari keshajipaka.Idiot

      Delete
  2. Kaka Salehe Umepaniki..Magazeti Kama Tanzania Daima kila Siku yanaandika Mbaya kuhusi serikali..We mwenyewe ni mnazi wa Simba..Watu hawasemi.Alafu Kah we unaakili kubwa Kwanini umepoteza Mda wako kuandika makala ndefu kuwajibu wadogo zako ambao wewe ndo ulianza kwa kuchukua Picha Zao na kuziweka kwenye blog yako..Usijione Uko sahihi braza..Hata Wao ni binadamu wanahisia wanafeeling za kufanya wanachotaka..Pole sana ulikosea kuwajibu..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa nilivyoelewa, baada ya kufikiria kwa makini (tofauti na wewe uliyekurupuka), Saleh hakuwa analenga kuonyesha kuwa ukiwa mwandishi wa habari ni dhambi kuwa mshabiki wa timu fulani, isipokuwa unatakiwa usionyeshe mahaba yako kwa jamii kwani wewe unaandika habari kesho kwa wanajamii wenye mapenzi na timu zote.

      Pia Saleh hajawajibu bali anawaonyesha wapi wamekosea (kama watakuwa na busara sitegemei wajibu waraka huu wa leo).

      Na kama hufahamu jombaa, tasnia ya habari ni nyeti na ina nguvu sana kwenye jamii so ni lazima tuwe na watu wenye maadili yanaoshabihi tasnia hiyo.

      Delete
  3. Kaka Salehe Umepaniki..Magazeti Kama Tanzania Daima kila Siku yanaandika Mbaya kuhusi serikali..We mwenyewe ni mnazi wa Simba..Watu hawasemi.Alafu Kah we unaakili kubwa Kwanini umepoteza Mda wako kuandika makala ndefu kuwajibu wadogo zako ambao wewe ndo ulianza kwa kuchukua Picha Zao na kuziweka kwenye blog yako..Usijione Uko sahihi braza..Hata Wao ni binadamu wanahisia wanafeeling za kufanya wanachotaka..Pole sana ulikosea kuwajibu..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Tumaini Benson naona naye ni wale wale. Naona hata hajui kwa nini Tanzania daima lazima waandike vitu vibaya kuhusu serikali. Hajui serikali ni ya CCM na Tanzania daima ni la CHADEMA?! Je hao waandishi nao wnatumikia vyombo vya habari ambavyo ni vya Yanga? Kama ndivyo basi waendelee kufanya wanachofanya na watakuwa sahihi. Kama sivyo nasi wanachemka mbaya. Wangekuwa wanatumikia gazeti kama la Mwanaspoti naamini wangeonywa

      Delete
  4. Salehe upo sahihi maana nimeanza kufuatilia mpira toka enzi za kina Charles Hilari na Ahmed Jongo na Mikidadi Maamudu na wengine na sikuwasikia wakisema wao wanapenda timu fulani. Upo sahihi naona kalamu imekosa mtumiaji. Hii ni michezo tukiwa ktk siasa wanaleta vita watu kama hawa.

    ReplyDelete
  5. WAANDISHI kama hawa ni wale wafanyabiashara 'MAKAHABA' wanaotumia kivuli cha uandishi wa habari kwa lengo la kujiuza na kujitongozesha kwa wachezaji wakiwa na maana ya kuwa wana mahaba na timu wanazochezea hao ambao wanawadhamiria na ndio maana wanakimbilia kuwavua mabwana zao medali na kuzivaa wao na kupiga nazo picha.
    Cha kuchekesha mwandishi mwenyewe ana sura tata na shepu tata kama mfereji wa maji taka.

    ReplyDelete
  6. Angekuwa mwandishi kweli nadhani tayari angekuwa keshaambatana na Yanga Angola na kuripoti mechi za kimataifa. Angesafiri na kuzijua nchi mbalimbali kama waandishi wengine sijui ingekuwaje na nina uhakika hana uwezo wa kusafiri hata kwenda Mbeya.Ndi ndi ndi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic