May 30, 2016


Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, Victor Wanyama anayekipiga Southampton ya England amekisifia kikosi cha Taifa Stars kwa kuonyesha soka safi huku akishangazwa kwamba hakukuwa na mchezaji hata mmoja wa kulipwa.

Stars ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya kwenye Uwanja wa Moi Kasarani  jijini Nairobi, jana na kutoka sare ya bao 1-1.

“Unasema leo hamkuwa na professional pale uwanjani?”  alionyesha kushangaa Wanyama.


 “Basi mna kikosi kizuri. Wengi ni vijana, wanaweza kama mkicheza kwa kutubana kama mlivyobana hapa, Misri mnaifunga na hata hao Nigeria, si ajabu nikasikia mnakwenda Afcon mwakani. Ninaitakia kila la khetri timu hii, nawatakiwa kila la kheri Watanzania katika harakati zao. 

"Sisi mwaka huu tumepotea kabisa, hatuna matumaini tena, tunajipanga ndiyo maana nimekuja kutetea taifa langu, hata kama tumekosa nafasi,” alisema Wanyama anayekipiga Southampton ya England.

Katika mchezo huo, Taifa Stars iliwakosa nyota wake Mbwana Samatta anayechezea Genk ya Ubelgiji kwa kuwa alikuwa na mchezo muhimu wa kupa nafasi timu yake ama icheze Ligi ya Uropa au ibaki nje katika michezo ya kimataifa ngazi ya klabu Ulaya. 

Shirikisho la Soka Tanzania na Kocha Mkwasa walimruhusu kama ilivyo kwa Thomas Ulimwengu anayekipiga TP Mazembe waliokuwa na mchezo mkali dhidi ya AS Vita ambao wana utani na ushindani mkali wa soka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


2 COMMENTS:

  1. Toka nikiwa mdg nmekuwa nkisikia hzo sentensi...hakuna mchezaji anaecheza nje (ulaya)
    Maisha yale yale stor zle zle

    ReplyDelete
  2. Toka nikiwa mdg nmekuwa nkisikia hzo sentensi...hakuna mchezaji anaecheza nje (ulaya)
    Maisha yale yale stor zle zle

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic