May 8, 2016


Yanga Bingwa.
Wameubeba ubingwa kwa mara ya pili mfululizo wakiwa na mechi tatu mkononi.

Msimu uliopita walibeba ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi, lakini safari hii wamechukua wakiwa na mechi tatu. Hii imetokana na Simba kupokea tena kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mwadui FC.

Kutokana na kipigo Yanga inabeba ubingwa ikiwa na pointi 68 ambazo hata kama Simba itashinda mechi zake tatu zilizobaki, itafikisha pointi 67 na Azam FC ikishinda mbili zilizobaki itakuwa na 66.



1 COMMENTS:

  1. Baada ya kuchukua ubingwa hatutaki kuona Yanga ikipanga matokeo na vitimu vidogo kama vile Ndanda,Majimaji na Mbeya City eti kuzisaidia zisishuke daraja.Hii ni aibu kubwa na viongozi watakaothubutu kushiriki njama hizo waripotiwe PCCB.Inashangaza viongozi kwa maslahi yao binafsi wako tayari kuvuruga rekodi ya Yanga ya kupoteza mechi moja msimu mzima au kufungwa siku ya kukabidhiwa kombe sababu tu wabinafsi Fulani wanataka kufaidika.Haya yalishatokea 2009 Yanga ilipofungwa mechi ya mwisho na 5-3 na Villa Squad iliyokuwa imeshashuka daraja na mwaka 2015 ambapo baada ya kuchukua ubingwa Yanga ililegeza na kufungwa 2-1 na Azam iliyokuwa inawania nafasi ya pili na pia katika mechi ya mwisho ya ligi Yanga ilifungwa 2-1 na Ndanda iliyokuwa inahitaji ushindi ili isishuke daraja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic