May 24, 2016


Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wamesema wanataka kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho na ikiwezekana wakutane na TP Mazembe.

Yanga imefuzu kuingia robo fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuivurumisha nje Esperanca ya Angola.

Timu wanazokutana nazo Yanga, tano zinatokea Kanda ya Kaskazini ambazo ni Mo Bejaia ya Algeria, FUS na Kawbab Marrakech (zote Morocco), Al Ahli (Libya) na Etoile du Sahel (Tunisia). Moja Kanda ya Magharibi ambayo ni Madeama kutoka Ghana na TP Mazembe ya DR Congo.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema wanatamani kukutana kwanza na timu za Waarabu.

“Zianze kwanza timu za Waarabu, zije tuzimalize zote baada ya hapo tuingie fainali.

“Kwetu TP Mazembe ni kama ndugu zetu, tunataka tukutane nao wakati tunachukua ubingwa katika fainali.

“Kuhusu Waarabu Yanga haina hofu tena hata kidogo hata wewe mwenyewe Saleh unalijua hilo. Mfano Al Ahly ambaye mbabe wa Waarabu alakini umeona alivyokutana na sisi,” alisema Muro akionekana kujiamini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic