June 13, 2016



Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Mkenya, Idd Salim, mwishoni mwa wiki iliyopita alihitimu mafunzo yake ya ukocha kwa ngazi ya diploma huko nchini Poland na kuweka rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza kwa mwaka huu kuhitimu masomo hayo barani Ulaya.

Mkenya huyo aliyeinoa Simba kwa takriban miezi sita kabla ya kufungashiwa virago Januari, mwaka huu, kwa sasa anawanoa makipa wa timu ya MFK Topolcany inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Slovakia.



Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Poland, Salim alisema katika mafunzo hayo, Mwafrika alikuwa peke yake na kuweka rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza kwa mwaka huu kufanikiwa kuhitimu masomo hayo yaliyofanyika kwenye Mji wa Brzeg uliopo Kusini Magharibi mwa Poland.

“Namshukuru Mungu kwa kuhitimu masomo yangu ya ukocha ngazi ya diploma ambapo tulikuwepo makocha wa makipa 100 pekee kutoka klabu mbalimbali hapa barani Ulaya kama vile BVB Borussia Dortmund, FC Porto, Sampdoria, Lipzig Red Bulls, Genk, FC Barcelona na Bayer 04 Leverkusen.

“Mafunzo yalianza Jumatatu ya Juni 6 na kumalizika Juni 9 na nimekuwa Mwafrika wa kwanza kwa mwaka huu kuhitimu masomo haya chini ya mkufunzi wetu, Milosz Gladoch,” alisema Salim.

Aidha kocha huyo, ameongeza kuwa kwa sasa hafikirii kurejea kufundisha soka barani Afrika kwani anaangalia kwanza anawezaje kufanikiwa akiwa barani Ulaya ndipo atarejea Afrika.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic