June 4, 2016


Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limeipiga faini Barcelona kwa kutumia bender za kisiasa katika moja ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barcelona imetwanga faini ya euro 150,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 345.

Mashabiki wa Barcelona walitumia bendera maarufu za Estelada ambazo ni maarufu kwa wale mashabiki wa siasa wanaotaka sehemu ya Catalunya kujitenga na Hispania.

Uefa imesema suala hilo ni la kisiasa na Barcelona wanajua suala hilo si sahihi. Hata hivyo wamepewa nafasi ya kukata rufaa.


Hivi karibuni, Barcelona ilipewa onyo wakati wa fainali ya Copa del Rey kuhakikisha hakuna matumizi ya bendera hizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic