June 1, 2016


SANGA (KUSHOTO) AKIWA NA MANJI.
Baada ya ukimya, sasa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na makamu wake, Clement Sanga wanachukua fomu za kugombea nafasi hizo, kesho.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema, Manji na Sanga watachukua fomu za kugombea tena nafasi hizo, kesho saa sita mchana.


“Ni kweli tuna taarifa hizo, maana siku ni moja tu na Manji na Sanga watajitokeza kesho,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Pamoja na TFF kutangaza uchaguzi "wake" wa Yanga, Uchaguzi wa Yanga chini ya klabu ya Yanga umepangwa kufanyika Juni 11 na ratiba kamili iko hivi.

Tarehe 1/6/2016. Kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.Mhusika/ Katibu Mkuu.

 Tarehe 2-3/6/2016. Kuanza kuchukua fomu za ugommbea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi. Mhusika/ wagombea wote

Tarehe 4/6/2016. Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea  na kuandika barua  za kuwajulisha wagombea  juu ya mchujo wa awali na kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha  ya awali ya wagombea. 

Mhusika/ Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.
Tarehe 5/6/2016. Kipindi cha kupokea na kuweka mapingamizi kwa mgombea. Mhusika/ Kamati ya uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.

Tarehe 6-7/6/2016 Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili  wa awali, kupeleka majina TFF ilikuhakikiwa, kusikilizwa na kutolea maamuzi ya masuala ya maadili na kukata rufaa kwa maamuzi yaliotolewa, Kusikilizwa  rufaa na kutoa maamuzi ya rufaa na kisha kutangaza majina ya wagombea. Mhusika /TFF.

Tarehe a7-10/6/2016 Kipindi cha Kampeni kwa wagombea. Mhusika/ Wagombea.

Tarehe 11/6/2016 Uchaguzi wa Yanga. Mhusika/ Wanachama

Tarehe 12/6/2016 Kutangaza matokeo. Mhusika/ Wote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic