June 1, 2016


Wakati baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamepumzika kutokana na kumalizika kwa pilika za michuano hiyo, suala hilo lipo tofauti kwa kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko aliyeamua kuanza upya mazoezi akiwa mapumzikoni kutokana na kibarua kilichopo mbele yake.

Kamusoko kwa sasa yupo kwao Zimbabwe lakini amekiri kuwa ugumu walionao Yanga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ndiyo umemfanya avunje mapumziko na kuendelea na ‘tizi’ kama kawaida.

Katika michuano hiyo iliyobakiza timu nane zilizotengwa kwenye makundi mawili, Yanga imepangwa na wababe TP Mazembe ya DR Congo, MO Bejaia (Algeria) na Medeama (Ghana).

Kamusoko anayetarajia kurejea nchini Juni 8, mwaka huu kuungana na timu amesema moja kwa moja kutoka Zimbabwe akifafanua zaidi kuhusiana na aina ya mazoezi anayofanya kwa sasa pamoja na michuano hiyo.


“Unajua kwenye makundi kutakuwa na kazi kubwa, unahitaji kuwa fiti zaidi kwa hiyo nimeamua kufanya mazoezi mimi mwenyewe kujiweka fiti zaidi kimwili.

"Sifanyi mazoezi ya kuchezea mpira, zaidi ninakimbia na kufanya ‘push up’ na ninafanya hivyo kila siku asubuhi na jioni, ” alisema Kamusoko mchezaji bora wa mwezi Desemba msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic