June 20, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Mwinyi anapewa kadi ya pili ya njano ambayo inazaa kadi nyekundu. Ilikuwa ni baada ya kucheza rafu kwa kumkwatua kwa nyuma mchezaji wa Bejaia

SUB Dk 85, Tambwe anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony
Dk 81 sasa, mechi imeanza kuchezwa. Bado Bejaia wanaonekana kucheza pasi nyingi na taratibu kwa lengo la kulinda lango lao.


Dk 79, Waarabu wanaanza vituko, taratibu kila mmoja anaanza kujiangusha kila baada ya dakika chache, ili kupoteza. Wale watu wa huduma ya kwanza na wenyewe nao wanaingia kwa mwendo wa maringo kabisa.
Dk 76, Yanga wanafanya shambulizi kali kabisa, Tambwe anaingia vizuri na kupiga krosi safi lakini MWashiuya anaipoteza hapa, hakutulia na ilikuwa nafasi nzuri kabisa kwa Yanga
SUB DK 72, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Mwashiuyaa

Dk 70, Twite anafanya kazi ya kuokoa na mpira unakuwa wa kurushwa
Dk 66, Yanga wanaonekana kuamka na kufanya shambulizi. Msuva anajaribu kuingia lakini Bejaia wanaokoa hapa
Dk 61, Yanga inapata kona ya kwanza, Msuva anachoka safi, Bejaia wanaokoa inakuwa kona nyingine, inachongwa tena na Msuva wanaokoa tena 
Dk 59, Msuva anapata nafasi lakini akiwa mbali ya lango, anapiga shuti kali kabisa, mpira unatoka juuu

Dk 57, Bejaia wanaonekana kuupoza mchezo, inawezekana wanataka kufanya shambulizi la kushitukiza
Dk 54, mpira unasimama kwa zaidi ya dakika moja hivi kwa kuwa mashabiki wanarusha fataki
Dk 53, Yanga wanacheza vizuri kwa kugongeana, Niyonzima kwake Tambwe, anamuachia KAseke lakini anapiga shuti mtoto kabisa
Dk 49, Bossou anakuwa mzito na analazimika kuutoa mpira na kuwa kona, imechongwa na kuokolewa, unakuwa mpira wa kurusha lakini wanatoa nje Bejaia na kuwa goal kick
Dk 47, mechi imeanza kwa kasi na Bejaia wanaonekana kuanza na ile kasi kama ya kipindi cha kwanza mwanzoni

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Ngoma analambwa kadi ya njano kwa kucheza madhambi, sasa wachezaji wawili wa Yanga wana kadi mbili za njano
Dk 43 Bejaia wanapata mpira wa adhabu wanauchonga lakini unaokolewa na mabeki wa Yanga na kuwa mpira wa kurushwa

Dk 41, Yanga wanapata kona lakini inachongwa haina manufaa. 
Dk 36 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja. Lakini Yanga wanaonekana kuwa makini ingawa wao hawajasukuma mashambulizi ya uhakika
SUB Dk 32, Haji Mwinyi anaingia kuchukua nafasi ya Oscar Joshua aliyeumia

Dk 30 Joshua anatolewa nje baada ya kuumia, anapata matibabu
KADI Dk 27, Twite analambwa kadi ya njano
Dk 26, mpira unasimama kwa muda kwa kuwa mchezaji mmoja wa Bejaia ameumia
DK 24, Tambwe anawekwa chini lakini mwamuzi anasema endeleeni

GOOOOOOO Dk 21 Bejaia wanaandika nao la kwanza kupitia Yacine Salhi ambaye aliunganisha krosi vizuri kabisa, na mashabiki wao wanasherekea kwa nguvu kabisa
Dk 19, kidogo Bejaia wanaonekana kuwa na kasi na kushambulia mara nyingi zaidi. Yanga wanalazimika kuwa makini na krosi za Bejaia maana wana watu warefu

Dk 18, kona inachongwa kwenye lango la Yanga lakini Bossou anaondosha hatari langoni
Dk 15, Kaseke anashindwa kuiwahi pasi nzuri kabisa. Kama angeiwahi, basi ingekuwa nafasi nzuri kwa Yanga
Dk 13, Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa kwa shuti kali la karibu kabisa

Dk 8, Ngoma anaingia vizuri anaangushwa hapa. Mwamuzi anasema ni faulo, Niyonzima anapiga vizuri kabisa lakini mabeki wa Bejaia wanaondosha
Dk 4, Bejaia wanaonekana kuwa na hamu ya kufunga kwa kuwa wanapiga pasi za haraka haraka lakini Yanga wako makini
Dk 2, Mechi imeanza kwa kasi na sasa ni dakika ya 2, Bejaia wanaonekana kuanza kwa kasi kulishambulia lango la Yanga.



KIKOSI:
1: Deo Did a
2: Mbuyu Twite
3: Oscar Joshua
4: Kelvin Yondani
5: Vicent Bossou
6: Thabani Kamusoko
7: Simon Msuva
8: Harouna Niyonzima
9: Donald Ngoma 
10: Hamic Tambwe
11: Deus Kaseke

SUBSTUTE:

- Ally Bathez
- Mwinyi Ngwali
- Pato Ngonyani
- Antony Matheo
- Juma Makapu

- Godfrey Mwashiuya

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic