June 27, 2016



Aliyekuwa mshambuliaji nyota wa Stand United, Elias Maguri amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Dhofar SC ya nchini Oman.

Maguri ambaye alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita kabla hajaanza kutoelewana na uongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, alisaini mkataba huo jana.

Klabu hiyo ndiyo wawakilishi wa Oman katika michuano ya Bara la Asia, hivyo hii itampa Maguri nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa zaidi.

Awali alikuwa akiwindwa na timu kadhaa ikiwemo Simba ya jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kujiunga nazo na kutimkia nchini Oman.

Kabla ya kwenda kwenye timu hiyo, Maguri ambaye alitoka Simba kabla ya kujiunga na Stand aliwahi kufanya majaribio kwenye timu ya TP Mazembe na kusema kuwa amefanikiwa kufuzu, ingawa klabu yake ilimgomea  kwa kuwa hakufuata utaratibu wakati wa kwenda kwenye majaribio hayo.


Msimu uliopita mshambuliaji wa huyo wa Taifa Stars, aliifungia timu yake mabao 15 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Amissi Tambwe (21), na Donald Ngoma (17).

3 COMMENTS:

  1. Bora angecheza kokote africa lakini sio kwa hao waarabu,tatizo kubwa la waarabu ni ulipaji kodi,mgeni unakuwa na vipengele vingi vya kodi mpaka unajuta.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic