June 10, 2016



Kwa hali ilivyo, Yusuf Manji atakuwa Mwenyekiti wa Yanga kwa miaka mingine minne, hilo halina ubishi kunapo uzima.

Hii inatokana na mambo mawili makuu, kwanza ndiye anakubalika zaidi kwa wanachama wa Yanga watakaopiga kura kwenye uchaguzi mkuu kesho.

Lakini ni mgombea pekee wa kiti hicho, hivyo anategemewa kuibuka kwa ushindi wa kishindi, akiishinda hewa.


Pamoja na uhakika huo, hiyo haijamzuia Manji kufanya kampeni yake mbele ya wanachama wa Yanga kazi iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo eneo la Jangwani, Kariakoo jijini Dar es Salaam.


 “Tuliingia na ahadi ya Simba, wakati huo timu ilikuwa na migogoro, viongozi waliokuwepo walikuwa wakilumbana hasa baada ya kufungwa mabao 5-0.

“Lakini mimi na Sanga (makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake) kwa kuwa tulikuwa na mawazo sawa, tulipigana na matunda yake ndiyo haya mnayoyaona,” alisema Manji.

Manji ambaye alikuwa akishangiliwa wakati akizungumza amesisitiza suala la Yanga kujitegemea na atalifanyia kazi.

Wagombea wengine katika nafasi ya ujumbe ni ni Ayoub Nyenzi, Lameck Nyambaya, David Ruhago, Salum Mkemi, Samuel Lukumy, Tobias Lingalangala, Beda Tindwa, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ na Hussein Nyika.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic