June 1, 2016


Timu ya taifa ya Misri, Pharaos, inatarajiwa kutua nchini leo Jumatano kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2017) dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Mchezo huo wa Kundi G unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar, ambapo utachezeshwa na mwamuzi Meya Bastred akisaidiana na Mihndou Gauthar na Vinga Theophil na mwamuzi wa mezani ni Oboga Eric, wote kutoka nchini Gabon.

Katika kundi hilo Misri ndiyo wanaongoza wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Nigeria wenye pointi mbili Tanzania ni ya tatu ikiwa na pointi moja, hivyo inahitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kufuzu.

 Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas, alisema kuwa kwa asilimia kubwa maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na wamejipanga vizuri kuwapokea wageni wao hao.

“Timu ya Misri watafika kesho (leo) lakini bado hawajatuambia muda gani watakuja, kila kitu kipo vizuri, huu ni mchezo muhimu kwa Srars kwani kwa vyovyote vile inatakiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo,” alisema Lucas.

Mbali na hilo Lucas pia alisema: “Timu yetu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, inatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kucheza mechi ya kirafiki, mchezo ambao unatarajiwa kupigwaJune 17 mwaka huu, watautumia mchezo huo kwa maandalizi ya mechi zao za kuwania kupata nafasi ya kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake hapo mwakani.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic