June 27, 2016

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kikosi cha Yanga kushuka uwanjani kukipiga dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, imefahamika kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ataukosa mchezo huo.



   Msuva ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga katika msimu miwili iliyopita, anasumbuliwa na malaria, hivyo kufikia kesho hatakuwa fiti kuweza kucheza mchezo huo wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
   Akizungumza na salehjembe, Kocha wa Yanga, Hans va Pluijm amekiri kuwa Msuva ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa mgonjwa na kudai kuwa anao wachezaji wengine wanaoweza kuziba nafasi yake.
  


Kukosekana kwa Msuva kunaweza kumpa nafasi kubwa kiungo mshambuliaji ambaye ni mgeni kikosini hapo, Juma Mahadh ambaye amesajiliwa akitokea Coastal Union ya Tanga kupangwa katika mchezo huo japokuwa anaweza kukutana na presha kubwa kwa kuwa siyo mzoefu katika michuano ya kimataifa.
Tayari TP Mazembe ipo jijini Dar, ambapo mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Jumanne kuanzia mida ya saa 10:00 Jioni huku Yanga ikiwa imetangaza kuwa mchezo huo utakuwa hauna kiingilio.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic