June 7, 2016

MWENYEKITI WA ZAMANI WA YANGA, NCHUNGA.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira Soka Tanzania (TFF) imeteua Kamati ya Leseni (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.

Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.

Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.

Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo inayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.


Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ni Wakili Alloyce Komba (Mwenyekit), Wakili Abdallah Gonzi (Makamu Mwenyekiti), Dk Francis Michael, Abdallah Mkumbura na Wakili Twaha Mtengela. Klabu zote zinahimizwa kuchukua fomu za maombi mapema ili kutoa muda wa kutosha kwa TFF kupitia maombi yao na kufanya uamuzi kwa wakati muafaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic