June 10, 2016


Kiungo mchezeshaji wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amemwambia beki wa timu hiyo, Hassani Kessy kuwa asahau maisha ya Simba na badala yake akili na mawazo yake aelekeza kwenye klabu yake mpya anaoichezea hivi sasa.


Kauli hiyo, aliitoa jana kwenye mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu ikijifua na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia utakaopigwa Juni 17, mwaka huu huko Algeria.

Kessy alisaini kuichezea Yanga wiki tatu zilizopita akitokea Simba iliyomaliza naye mkataba wa kuichezea timu hiyo akitua Jangwani kwa dau la Sh milioni 40.


Niyonzima alisema, Kessy ni bonge la mchezaji, lakini kikubwa anachotakiwa ni kuzoea mazingira haraka ya timu, pia aendane na kasi ya Yanga ili apate nafasi ya kucheza.

Niyonzima alisema, pia beki huyo anatakiwa kupambana ndani ya uwanja pale atakapopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ili amshawishi kwa kumuani hapo baadaye.

“Nikwambie kitu, Kessy ni bonge la mchezaji na ni kati ya mabeki ninaowakubali kabla ya kusaini kuichezea Yanga, kikubwa anachotakiwa ni kupambana ndani ya uwanja ili apate nafasi ya kucheza.

“Pia, kingine kikubwa anatakiwa kufahamu yeye bado mdogo, hicho ndiyo kipindi chake muafaka cha kutengeneza maisha kwa kutumia soka, hivyo anatakiwa kuongeza mazoezi ili atengeneze soko lake,” alisema Niyonzima.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic