June 3, 2016


Timu ya taifa ya Misri kesho inatarajia kuumana na Taifa Stars katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), itakayofanyika huko Gabon mwaka 2017, lakini ujio na taarifa za ubora wa nahodha wa Stars, Mbwana Samatta zimekuwa zikikivuruga kikosi hicho.

Stars yenye pointi moja itapambana na  Misri yenye nne katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ikihitaji matokeo ya ushindi kwa ajili ya kujiweka katika mazingira mazuri.

Ingawa katika mchezo wa kwanza Mafarao hao walifanikiwa kuifunga Stars ikiwa ugenini mabao 3-0, lakini bado wamekuwa na wasiwasi kulingana na kiwango cha Stars na hasa Samatta anayeonekana kung’ara akiwa na timu yake mpya ya KRC Genk ya Ubelgiji, akiwa ameshaifungia mabao matano mpaka sasa.

Katika mazoezi waliyofanya juzi jioni kwenye Viwanja vya Gymkhana, Dar, baadhi ya waandishi wa habari walioongozana na timu hiyo walikuwa wakiulizia taarifa za Samatta kuhusu ujio wake kila wakati na kutaka kujua kama kuna baadhi ya wachezaji wenye kiwango kama chake ambao hawajasikika lakini wapo Stars.

Moja ya maofisa wa Shirikisho la Soka la Misri (Efa) ambaye hakujitambulisha jina lake aliwauliza waandishi wa gazeti hili kuhusiana na Stars: “Vipi Samatta amekuja? Tunamfahamu yule tangu yupo TP Mazembe (DR Congo), tunajua kiwango chake na ndiyo ambaye tunajua atatusumbua.

“Lakini kocha amejipanga na anajua tutafanya nini katika hilo, vipi lakini wachezaji wengine? Kama Samatta atakuwa na kiwango kile tunajua lazima kutakuwa na wengine wazuri pia hapa labda tu hawajasikika bado,” alijaribu kujieleza ofisa huyo.


Samatta amejiunga na Stars iliyo chini ya Boniface Mkwasa jana usiku akitokea Ubelgiji wakati Thomas Ulimwengu anayekipiga Mazembe yeye alishatua tangu juzi, tayari kwa mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic