June 29, 2016


Yanga imeshindikwa kutimiza ndoto yake ya kuwamaliza vigogo wa Afrika TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0.

Katika mechi hiyo ambayo mashabiki waliingia bure kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga imelala kwa bao hilo la dakika ya 75, mfungaji akiwa ni Merveillw Bope, lakini mchambuzi maarufu nchini Bakari Malima, amesema ni tata na linaonyesha ni offside.

Malima aliyekuwa beki nyota wa Yanga, Simba na Taifa Stars, amesema kuna utata wakati Bope akifunga bao hilo kwa kuwa alikuwa mbele ya wachezaji wote wa Yanga lakini pia akawalaumu walinzi wa Yanga.

“Ukiangalia kuna utata, naona ni offside kwa kuwa mfungaji alikuwa mbele. Unaona kabisa anamalizia wakati akiwa peke yake kabisa na mbele.

“Lakini pia walinzi wa Yanga hawakuwa makini kwenye kukaba, walikaa mbali. Wakati mwingine ni vizuri kukaba tu na kuondoa utata wowote utakaotokea,” alisema Jembe Ulaya.


Picha za video ambazo ‘zilikamatwa’ na kuwa mnato zinaonyesha Bope akifunga mbele ya mabeki wote wa Yanga.

Pamoja na kwamba kiungo Thabani Kamusoko alichelewa kuondoka kwenye ukuta, lakini Bope bado anaonekana yu mbele yake wakati akimalizia.

Mabeki wa Yanga, Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Kamusoko mwenyewe, mshambuliaji Donald Ngoma pamoja na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wanaonekana wakiinua mikono juu wakipinga kwamba mfungaji alikuwa ameotea.

Lakini picha hizo pia zinaonyesha kuna tatizo la ukabaji kama ambavyo Malima amesema, kwamba mfungaji alibaki peke yake na baada ya piganikupige, akamalizia kwa urahisi kabisa akiwa karibu na Dida.

Hata hivyo, Yanga iliweza kuonyesha soka la kuvutia na kuwapa TP Mazembe wakati mgumu huku Mtanzania, Thomas Ulimwengu akionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Yanga.

Yondani ndiye alimwangusha Ulimwengu nje kidogo ya boksi. Baada ya hapo faulo ilipopigwa, Yanga walionekana kama kuzubaa ingawa bado Bope kuwa mbele ya mabeki hao ndiyo kunazua utata huo.

Yanga ilipoteza nafasi kadhaa kama ilipokuwa kwa TP Mazembe ambao walionyesha uwezo mkubwa hasa katika safu ya ulinzi ambayo iliwathibiti vizuri washambulizi wa Yanga kama Ngoma, Obey Chirwa na Juma Mahadhi ambaye alionyesha kiwango cha juu.






3 COMMENTS:

  1. HAKUNA OFFSIDE yoyote pale. offside inapimwa wakati mtoa pasi anapiga mpira. wakati pasi inapigwa Kamusoko alikuwa kaua offside, na hata wakati mfungaji anaanza kupiga mpira walikuwa wako sawa na kamusoko. naweka link hapa na unatishe hiyo video wakati pasi imepigwa uone kama kuna offside. link hii hapa https://www.youtube.com/watch?v=shOgXok12YA

    ReplyDelete
  2. Pale yanga walibanwa, kwanza kumwangusha Uli..ile ingawagharimu na kuwa penati, sema tu mwamuzi alifumba jicho moja. Mpira wetu upo mdomoni sana!

    ReplyDelete
  3. Mimi ni mpenzi sana wa Yanga ila pale hakukuwa na offside kabisa.
    Offside ni wakati pasi inapigwa sio wakati wa kufunga.
    Ina maana hata Malima pamoja na kucheza mpira hajui Offside inakuwaje???
    Shame..

    Mythbuster

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic