June 1, 2016



Azam FC ipo kimya katika suala la usajili wa wachezaji wapya lakini taarifa inaeleza kuwa timu hiyo inajipanga kuwapiga panga jumla ya wachezaji 10 katika kikosi hicho.

Ukiachana na vuguvugu la mchezaji wao nyota, Muivory Coast, Kipre Tchetche, anayejipanga kutaka kuihama timu hiyo, lakini pia suala la kupunguza wachezaji hao limeelezwa kuzingatiwa kwa vigezo vya wale waliocheza chini ya kiwango na walioshindwa kufikia malengo ya timu hiyo msimu uliopita.

Mtu wa ndani kutoka klabuni hapo ameeleza kuwa mpaka sasa idadi ya wachezaji hao 10 tayari imepitishwa ingawa imekuwa ni siri kubwa juu ya listi ya majina ya watakaotemwa ikizingatiwa kupatikana kwa mbadala wa nafasi zao kwanza.

“Listi ni wachezaji 10 na kuna asilimia kubwa ikagusa mpaka wachezaji wa kimataifa, lengo ni kurekebisha upungufu mwingi wa msimu uliopita na kuingiza watu wapya wa kazi. Majina ni ngumu kwa sasa kuwekwa hewani, ikizingatiwa katika ufanisi wa kuwapata mbadala wao kwanza,” kilisema chanzo hicho.


Aidha, alipotafutwa Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd kuzungumzia suala hilo, alisema: “Kwa sasa timu ipo likizo na uongozi unafanya mambo mengine, tukishaingia kwenye suala la usajili kama ni kuacha au kuongeza tutawaambia tu."

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic