July 24, 2016


Wakati kocha Jose Mourinho akipambana kumnasa Paul Pogba, inaonekana wazi kuwa kiungo mkongwe Bastian Schweinsteiger ataongoza kundi la ambao watatemwa.

Tayari Mourinho amefanikiwa kumsajili mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic pia  Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan ambaye pia ni kiungo, hivyo nafasi ya Schweinsteiger inakuwa ndogo.

Lakini kuna wengine walio kwenye hofu ya kutupiliwa mbali ingawa bado kuna viungo watakuwa na nafasi kama Morgan Schneiderlin, Michael Carrick, Ander Herrera na Marouane Fellaini. 

Wako wenye hofu kama Marcos Rojo, Juan Mata, Matteo Darmian, Memphis Depay, Adnan Januzaj na Ashley Young ambao inaonekana wanaweza kubaki lakini hawana uhakika wa asilimia mia.


Uhakika wataondoka:
Bastian Schweinsteiger
Marcos Rojo 
Matteo Darmian

Bado hawana uhakika 50/50:
Juan Mata 
Memphis Depay 
Adnan Januzaj
Ashley Young

Uhakika wanabaki Old Trafford:
Marcus Rashford
Guillermo Varela 
Will Keane
James Wilson 

Tyler Blackett

3 COMMENTS:

  1. Ifike mahali sasa uwe unatupatia na chanzo cha habari yako,hatuwezi kuendelea kulishwa matango pori bila kujuwa yametoka wapi na yamelimwa na nani.

    ReplyDelete
  2. Mmmmmmmh kaka mbona unaferi sasa,huyo varela mbona kashatolewa kwa mkopo(frankfut),na huyo blackett hata pre season ayupo na ajashiriki EURO ?

    ReplyDelete
  3. Mmmmmmmh kaka mbona unaferi sasa,huyo varela mbona kashatolewa kwa mkopo(frankfut),na huyo blackett hata pre season ayupo na ajashiriki EURO ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic