July 2, 2016



Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetupilia mbali shauri la Msemaji wa Yanga, Jerry Muro kusikilizwa.

Kamati hiyo imesema hoja zilizotolewa ili kumuita Muro zilikuwa na mapungufu na haikuona kama kuna sababu ya kumuita na kumhoji.

“Kweli kamati ya maadili imetupilia mbali, ninaona ni ushindi kwa Wanayanga na ninawasamehe wote walionitesa.

“Huu ni ushindi wa Wanayanga wote, lakini wito wangu kwa sasa ni sote kuungana, kwa Wanayanga na TFF kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini,” alisema Muro katika ujumbe wake mfupi.


Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Wilson Ogunde alisema TFF inapewa nafasi ya kumpa Muro wito mwingine kama utaona anatakiwa kweli kuitwa kwenye kamati hiyo.

"Kama TFF inahitaji aitwe tena, basi tuwape nafasi ya kumuita tena kwa barua nyingine ukiachana na ile ambayo ilionekana kuwa na mapungufu," alisema Ogunde.

Jerry aliitwa kwenye kamati ya maadili baada ya TFF kupitia katibu wake mkuu, Mwesigwa Celestine kumtumia barua hiyo ya wito ingawa nayo ilikuwa na mpungufu rundo kwani haikueleza hata anatakiwa katika kamati ipi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic