July 13, 2016



Simba imeonyesha kuwa haitaki masihara na imepania kurejesha ilichopoteza kwa misimu minne mfululizo baada ya kubadili upepo wa programu nzima ya kujifua katika kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro.

Simba ambayo iliondoka Jumapili iliyopita ikiwa inafanya mazoezi yake kwa siku mara moja katika kipindi cha wiki iliyopita, sasa imeanza kazi kweli kwa kufanya mazoezi kwa siku mara mbili; asubuhi na jioni.

Ikiwa chini ya kocha mpya timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog, kikosi hicho pia kimeelezwa kuwa kwenye morali kubwa huku wakichagizwa na deni walilonalo kwa mashabiki na viongozi la kutonyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu minne sasa.

Nahodha wa Simba, Musa Mgosi ameliambia Championi Jumatano kuhusiana na hali iliyopo kambini hapo huku akitaja pia ujio wa wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni umekuwa ukimpa matumaini makubwa ya kufanya mapinduzi katika Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2016/17.

“Huku kwa sasa tunafanya mazoezi mara mbili, asubuhi, tunapumzika mchana kisha jioni kama kawaida. Mazoezi ya kocha ni mazuri na yanajenga kwa kipindi hiki ambacho tumetoka mapumzikoni, siwezi kukutajia ni ya aina gani lakini yanatujenga hasa.


“Wachezaji wapya pia wametuongezea nguvu na uzuri kila mmoja hapa anafahamu kwamba tuna deni kubwa kwa mashabiki, wanachama, viongozi na wote wanaoipenda Simba,” alisema Mgosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic