July 9, 2016



Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ haishiwi vituko na safari hii ameibuka na kusema anataka kuwa na wachezaji ambao wanaweza kucheza muda wowote na siyo wasiotumika.

Hii ya Julio inafanana na ile staili ya Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli ambaye anaendesha zoezi la kuwabaini watumishi hewa ambao wanalipwa na serikali lakini hawapo kazini.

Sasa Julio anataka kila mchezaji atakayekuwa naye kikosini ni lazima awe tayari kutumika muda wowote na siyo kuwa na kikosi cha kwanza cha kudumu huku wengine wakiwa ‘wazee’ wa benchi.

Kutokana na hilo, Julio amepanga kuwa na wachezaji wasiozidi 23 kwani anaamini hao ndiyo wanaweza kuwa na nafasi za kucheza mara kwa mara kwa kupokezana.
Kwa kawaida timu ya Ligi Kuu Bara inatakiwa kuwa na wachezaji kuanzia 25 mpaka 30.


Julio amesema kuwa: “Timu yangu itakuwa na wachezaji 23 kwani sitaki kuwa na rundo la wachezaji ambao sitawatumii kama watumishi hewa. Kikosi changu kitakuwa na makipa watatu na wachezaji wa ndani 20 basi."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic