July 20, 2016


Mara baada ya kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora kwenye msimu wa Ligi Kuu Bara 2015/2016, beki wa Yanga, Juma Abdul ametaja siri tatu za yeye kufanikiwa kuchukua tuzo hiyo.

Abdul alifanikiwa kuchukua tuzo hiyo, akimpita Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kutoka Simba na kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya (ambaye ametua Simba), huku akichota Shilingi 9,228,820.

Abdul amesema siri kubwa za mafanikio yeye kushinda tuzo hizo ni muda mwingi alioutenga kwa ajili ya kupumzika na siyo kufanya starehe kama walivyokuwa wachezaji wengine.

Alisema sababu nyingine ni, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja ikiwemo kutimiza majukumu yote anayopewa na kocha wake Mholanzi, Hans van Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Alimalizia kwa kutaja kuwa ni kujituma kwake ndani ya uwanja kumemsaidia yeye kushinda tuzo hiyo ya uchezaji bora huku akiahidi kuendelea kupambana kwenye msimu ujao ili aichukue tena kwa mara ya pili tuzo hiyo.

“Haikuwa kazi rahisi kwangu mimi kushinda tuzo hii niliyoshinda ya uchezaji bora kwenye msimu huu, kiukweli nilijitahidi kufuata kanuni zote za mchezaji ambazo mchezaji anahitaji kuwa nazo.

“Nazo ni kupata muda mwingi wa kupumzika kwa maana ya kulala ili kupumzisha mwili mara baada ya kutoka mazoezi na siyo kwenda kufanya starehe kama ilivyokuwa kwa wachezaji.


“Nilijitambua na kutimiza majukumu yote niliyokuwa nikipewa na kocha kabla na baada ya mechi kuhakikisha ninacheza kwa kiwango cha hali ya juu, pia nidhamu yangu ilichangia kwa kiasi kikubwa,”alisema Abdul.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic