July 23, 2016


Baada ya kuwa kambini kwa wiki mbili, Simba chini ya Kocha Joseph Omog, leo Jumamosi inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro 'Mji Kasoro Bahari'.

Simba imepanga kucheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Burkina Fasso na Polisi Morogoro zote za Ligi Daraja la Kwanza. Mechi mbili ni dhidi ya Burkina Faso na moja dhidi ya Polisi Morogoro.

Ikiwa kambini Morogoro, Simba imeendelea kupokea wachezaji mbalimbali kwa ajili ya majaribio kabla ya kusajiliwa na tayari wachezaji wanne wa kigeni wametimuliwa kwa kutofikia viwango.

Mmoja wa viongozi wa Burkina Fasso, Franky Julius anayeratibu mechi hizo, alithibitisha kucheza michezo miwili ya kirafiki kuanzia na ule wa leo Jumamosi.
Julius alisema, baada ya mechi hiyo, Simba itacheza mchezo mwingine wa kirafiki uwanjani hapo kesho Jumapili dhidi ya Polisi Morogoro.

Alisema Burkina Faso itacheza mchezo mwingine wa mwisho wa kirafiki na Simba huko Kilosa, Morogoro wiki ijayo.

“Kama kiongozi wa Burkina Fasso na mratibu wa mechi zote, tumepanga kucheza mchezo wa kirafiki na Simba kesho (leo), halafu Jumapili (kesho) Simba watacheza mechi nyingine na Polisi Morogoro kabla ya kucheza mchezo mwingine wa kirafiki wiki ijayo,” alisema Julius.


Meneja wa Simba, Abbas Ally, alithibitisha uwepo wa mechi hiyo ya Simba leo kwa kusema: “Jana (juzi Alhamisi) hatukucheza mechi yoyote ya kirafiki tofauti na watu walivyokuwa wanavumisha, kiukweli tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu na lengo ni kocha kuona uwezo wa kila mmoja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic