July 8, 2016





Mshambuliaji nyota wa Azam FC, Kipre Tchtche bado hajarejea nchini na kujiunga na wenzake baada ya mapumziko yake.

Hajatoa taarifa na inaelezwa anaweza kukumbana na adhabu kama itabainika hakuwa na sababu za msingi.

Kabla ya kwenda kwao Ivory Coast baada ya msimu kwisha, Tchetche alisafiri hadi Dubai ambako alifanya mapumziko safi na familia yake.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amesema wanafanya kila njia kupata sababu za mshambuliaji wao, Muivory Coast, Kipre Tchetche kutorejea kikosini mpaka jana kinyume na taratibu ambapo alitakiwa kuwa kikosini. 

“Kipre bado ni mchezaji wetu, ana mkataba wa mwaka mmoja hivyo hawezi kwenda popote na bahati nzuri hata ITC yake tunayo sisi, kwa hiyo tunajaribu kufanya mawasiliano kujua sababu ya kuchelewa kambini na kinyume cha hapo atachukuliwa hatua,” alisema Idd.


Naye pacha wa nyota wa Kipre, Michael Bolou alipoulizwa na gazeti hili kuhusu alikomuacha mwenzake alijibu kwa kifupi: “Mimi nilimuacha nyumbani, mengine sifahamu lolote."

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic