July 17, 2016


Hiki ndicho alichoandika na ninakitupia kama kilivyo ili upate ladha yale.

A.aleikum

  Awali ya yote nianze kwa kumshukuru mungu.mwingi wa rehma zote.
Ni wiki mbili kamili zitakazotimia leo usiku.majira ya saa nane usiku.muda huo bila shaka ntakuwa ktk anga la dunia nikisafiri kuelekea New Delhi India kupitia muscat Oman.kwa ajili ya matibabu yangu ya macho.

Usiku wa siku kama ya leo jpili ya tarehe 3-7-2016 nilistuka usiku kwa ajili ya daku.ndipo nilipogundua jicho langu la kushoto halioni kabisa.na jicho langu la kulia lina uoni mdogo.
Ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu.

Najua madaktari mbali mbali wa hapa nchini walifanya kila jitihada za kunusuru macho yangu ila bado ufumbuzi wa tiba yangu bado haujapatikana.na ndio maana naenda kujaribu India.na inshaallah mungu atanivua mtihani huu.

Kiukweli hawa madaktari niwashukuru sana kwa jitihada zao.
Rafiki yangu na kaka yangu dr Mohammed wa wizara ya afya.
Dr Mahunda wa ocean Road.
Dr Dalla.Dr Chibuga na Dr Hassan wa CCBRT
Dr Datoo wa clinic ya pale shoppers plaza.mikocheni.
Madaktari wa kituruki pale ktk hospitali yao ya international eye clinic maenoe ya moroco.pamoja na wauguzi wao.
Mungu atawalipa inshaallah

Kipekee niwashukuru ndugu na rafiki zangu wa KT. Hapa mm ndio maskani yangu jioni.
Hawa ni zaid ya binadaam.kisasa tungesema show nzima ya safari wanasimamia wao.
Wamefanya jitihada zote na kiukweli bila wao sijui ingekuwaje.

Kwa wiki zote mbili wamekimbizana na mm ktk ugonjwa wangu.

Pia niishukuru ofisi yangu klabu ya Simba.ni zaid ya wema walionifanyia.

Niwashukuru viongozi wote. friends of Simba.wanachama na wapenzi wote wa unyamani.kwa kila jambo na dua zao walizonifanyia.
Kiukweli sijutii kupenda na kufanya kazi Simba.

Niishukuru pia serikali ya nchi hii. nimepokea salaam kutoka kwa waziri wangu wa michezo.Mh Nape.salaam toka kwa waziri na naibu waziri wa afya.Mh Ummi na mh kigwangala.
Salam toka kwa rafiki zangu manaibu waziri Mh Mavunde na mh Posi.

Lakini kipekee kwa waziri wangu wa mambo ya ndani ya nchi.mtani wangu Mh Mwigulu Nchemba ambae yy mwenyew alikuja kuniona na kwa niaba ya serikali wameahidi kunisaidia kwa kila hali niweze kupona.
Na kwa hapa nisiache kumshukru mwambata wetu wa afya ktk ubalozi wetu nchini India. Dr Goroka kwa kusaidia kupatikana kwa hospitali India.

Pia nimshukuru professor Janabi wa hospitali ya moyo Muhimbili kwa ushauri wake wa kitaalam.sambamba na daktari wetu wa Simba.

Sitatenda haki kama sitawashukuru viongozi wakuu wa Tff.rais Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa kwa kila jambo walilonifanyia

Kipekee niwashukuru viongozi wa dini.mashekh na maustaadh kwa dua zao kwangu.sambamba na wachungaji ambao walikuja hadi kwangu kuniombea..asanteni watu wa mungu.

Nisisahau kuwashukuru watani zangu Yanga.kwa mchango wao kwangu. Hususan mropokaji 😃😃 wao Jerry Muro.

Nitammiss sana kwa fujo na kebehi zake.
Ninamuomba awaandikie Tff kuomba radhi na kisha yy ajirekibishe kidogo.

Nna imani Tff nao wanaweza kupitia kamati zao wanaweza kuangalia namna sahihi ya kulimaliza hili kwa maslah ya mpira wa miguu nchini.
Muhimu jerry apime tu kauli zake.

Mpira si kashfa wala kebehi za kuudhi..na si uadui hata kidogo.

Mwisho niwashukuru ndugu zangu wa kkoo..
Hawa ni Alfa na Omega kwangu.kuanzia niliokuwa nao vjana wa Al -ahly.hadi kkoo family group.kfg

Pamoja nao watu wangu wa nguvu.watsapp groups ambazo zimeniombea sana na kunifariji ktk kipindi hiki kigumu.sambamba na kuja kunijulia hali.

Nikiwasahau wanahabari nitakuwa wa ajabu..wamefanya kazi kubwa ya kuwahabarisha na kuwapa maendeleo yangu kila siku kupitia vyombo vyao.

Asanteni sana wote.my family.ndugu zangu.jamaa na marafiki wote.nimejua kwa sasa Haji nna watu na nnamuomba mungu niendelee hv hv na tabia zangu njema nizilojaaliwa na Manani.

Msiache kuniombea kwa kila hatua.kuanzia safari yangu.matibabu na kuiombea familia yangu inayobaki hapa nyumbani.

Nawapenda sana.mungu awabariki sana.


Haji S.Manara

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic