July 29, 2016


Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema hatakubali kwa mara ya tatu kuona uongozi wake ukimaliza msimu wa tatu madarakani huku ikiukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao sasa unashikiliwa na Yanga.

Aveva amesema kuwa kinachotarajiwa kutokea sasa ni vita ya kupambana kurejesha heshima ya Simba baada ya kuukosa ubingwa wa ligi hiyo kwa miaka minne mfululizo huku Yanga ikitawala, ikifuatiwa na Azam FC.

Simba ambayo ipo chini ya Kocha Mcameroon, Joseph Omog, tayari imeanza mikakati ya nguvu kuelekea msimu wa 2016/17 kwa kuweka kambi ya pamoja huko mkoani Morogoro.

Aveva amesema hawana sababu ya kushindwa kuchukua ubingwa huo kutokana na maboresho makubwa waliyoyafanya ya benchi la ufundi pamoja na usajili unaoendelea kufanywa chini ya Omog waliyempa majukumu ya kupendekeza wachezaji wa kuwasajili.

Aveva amesema kwa kuanzia tayari kambi inaendelea kwa mazoezi ya nguvu huku wakitarajiwa kuwafanyia mashabiki wao ‘sapraizi’ katika siku ya Tamasha la Simba Day, Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.


“Tutawatambulisha wachezaji wetu wote tuliowasajili, achaneni na maneno ya mtaani na tetesi, subirini siku ya Simba Day mtajua kila kitu,” alisema Aveva aliyeongeza kuwa siku hiyo watatambulisha jezi zao mpya za nyumbani na ugenini kwa ajili ya msimu huo ujao.

1 COMMENTS:

  1. Magazeti na viongozi wetu Vs hatma ya timu zetu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic