July 30, 2016


Azam FC chini ya Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania, leo Jumamosi inacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Jang’ombe kwenye Uwanja wa Amaan.

Azam imejichimbia visiwani Zanzibar kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, tayari imeshacheza mchezo mmoja wa kirafiki juzi Jumatano dhidi ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Zeben atautumia mchezo huo kwa ajili ya kuangalia viwango vya wachezaji wa timu hiyo ili kupata kikosi chake cha kwanza.

“Kesho (leo) Jumamosi tutacheza na timu ya Taifa ya Jang’ombe mechi ya kirafiki kama alivyotaka kocha lengo likiwa ni kuwaangalia wachezaji wake na kujua nani ataanza kikosi cha kwanza.

“Pia kocha atautumia mchezo huu kutazama uwezo wa wachezaji wa kigeni ambao wanafanya majaribio kwenye timu yetu, lakini tunaweka utayari kwa wachezaji wetu kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga,” alisema Jaffar.


Azam ambayo ilishika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa ligi kuu, itacheza na Yanga Agosti 17, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic