July 2, 2016


Italia ni kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Euro. Lakini leo ni lazima wakivuke kisiki kigumu zaidi, Ujerumani.

Wanacheza mechi ya robo fainali dhidi ya Ujerumani lakini nao lazima wauvunje mfumo wa Waitaliano wa ulinzi.

Italia inaposhambuliwa imekuwa na watu nane kwa kuwa mabeki wa pembeni huingia ndani na kuwa mabeki wa kati na viungo halafu mawinga wanashuka na kuwa walinzi.
Mfumo huo unawafanya wanakuwa wagumu kufungika kutokana na kujaza watu wengi katikati ya uwanja.

Hata inapopigwa krosi, bado wao wanakuwa na nafasi zaidi ya kuuwahi mpira na kuokoa.

Wanaposhambulia, washambuliaji wao wa kati hutambaa pembeni kama mawinga na kupigiwa mipira mirefu.


Mfumo huo wa Kocha Antonio Conte unaifanya Italia kuwa moja ya timu ngumu kufungika. Je, Ujerumani wataupasua mfumo huo?

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic