July 9, 2016


ILI kujenga nidhamu ndani ya kikosi chao, Azam FC imeweka sheria ndogo ambayo mchezaji atakayechelewa mazoezini atapigwa faini ya dola 50 ambazo ni sawa na Sh 107,168.

Azam ambayo juzi Alhamisi ndiyo imeanza maandalizi ya msimu ujao, imepiga kambi kwenye hosteli zao zilizopo katika uwanja wao wa Azam Complex jijini Dar.

Mara baada ya kumaliza mazoezi ya jana asubuhi, kocha msaidizi wa kikosi hicho, Denis Kitambi aliwatangazia wachezaji wote kuwahi uwanjani dakika 15 kabla ya kuanza kwa mazoezi ya jioni yaliyoanza saa 9:00 jioni.

“Atakayechelewa lazima apigwe faini ya dola 50, si masihara kama kuna mtu atadhani utani basi achelewe ili aone kitakachotokea,” alisema Kitambi.

Azam pia kupitia maagizo ya kocha wao mpya, Zeben Hernandez itaanza mpango wa kurekodi vipindi vyote vya mazoezi kisha baadaye vitakuwa vinapitiwa ili kutazama ufanisi wa kila mmoja wao.

“Nataka mazoezi yetu yarekodiwe picha za video halafu baadaye natazama ufanisi wa kila mchezaji ili kukifanya kikosi kuwa bora zaidi,” alisema Hernandez raia wa Hispania.

Hernandez pia ametoa siku 15 za kuangalia uwezo wa wachezaji wake kabla hajatangaza jeshi lake la msimu ujao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic