August 1, 2016

CHANDE MAHARAGE
Kampuni ya Multchoice Tanzania Dstv imetangaza kuonyesha Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil.


Michezo hiyo, inayoshirikisha aina michezo mbalimbali huku Tanzania ikiwakilishwa na  Riadha, Judo na Kuogelea yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 5 hadi21, mwaka huu.

Akizungumza wakati wakiwaaga wanamichezo wa Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema lengo kubwa ni kuwapa nafasi Watanzania kuwaangalia wawakilishi wao wa Riadha, Judo na Kuogelea waliokwenda katika mashindano hayo.

"Jumla ya Channel saba ambazo tumeziongeza zitaonyesha Olimpiki huko nchini Brazil na kikubwa zaidi tunataka kuwapa nafasi Watanzania kuwaangalia wawakilishi wetu waliokwenda kutuwakalisha," alisema Chande.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura alisema kuwa :"Kwanza kabisa ningeanza kwa kuwapongeza Dstv kwa kujitokeza kila wakati katika kuinua michezo hapa nchini.

"Hilo ni jema kwetu, ninaomba niwatie moyo tu, milango ipo wazi kujitokeza kila wakati pale mtakapohitaji kitu kutoka Serikalini." 




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic