August 14, 2016



Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema watu wanaweza kushangazwa na Simba kuwaacha washambuliaji wake wanaong’ara kwenye Ligi Kuu Bara lakini kumekuwa na sababu tofauti huku akisema Hamisi Kiiza, alikuwa tatizo na mtengeneza matatizo ndani ya kikosi cha Simba.

Manara amemtaja Kiiza kama chanzo cha matatizo, asiye mvumilivu na mbinafsi kupita wachezaji wote waliowahi kuichezea Simba.

“Kiiza kweli alifunga mabao 19 kwenye ligi, lakini kwa aina ya uchezaji wa Simba angefunga hata zaidi ya 25. Lakini tabia yake ni mtu muanzisha matatizo, ni tatizo kubwa kuliko unavyofikiri.

MANARA

“Kila mara alikuwa anaanzisha migogoro, mshahara ukichelewa siku tatu anaanza kulaumu. Mfano kuna siku nilikwenda mazoezini kwa niaba ya uongozi kuwaeleza wachezaji kuwa mshahara tayari umeingizwa benki.

“Nikawasubiri wamemaliza mazoezi, wakaambiwa ninataka kuzungumza naye. Wakati naanza tu kuzungumza, yeye akarukia na kuanza kusema mishahara leo ni tarehe tatu, anasikitika sana. Nikamuuliza unajua kilichonileta hapa? Vipi hausikilizi hata kiongozi anachoongea halafu nawe useme yako.

“Ni mtu asiye na subira, tukifika hotelini anataka chumba chake kiwe tofauti na wengine. Anataka achelewe kuja kula, lakini awekewe. Anataka kwenye basi achelewe, limsubiri. Kwa kifupi ni mtu anayeua morali ya wachezaji kwa kiwango cha juu kabisa.


“Nikuhakikishie kama Kiiza angebaki msimu huu, mimi ningeondoka. Maana kungekuwa hakuna haja ya kupambana halafu ndani ya timu kuna ‘kirusi’ kinawatafuna,” alisema Manara.

"Kuhusiana na Amissi Tambwe, ukweli ule ulikuwa ni mfumo wa mwalimu Phiri, ilionekana haendani na mfumo naye akaamua aondoke.

"Alikuwa akimuweka benchi na akiingia hafanyi vizuri hata katika mechi za kirafiki. Uongozi ulimuamini kocha ndiyo maana ukatekeleza alichosema," alisisitiza Manara.

1 COMMENTS:

  1. Kiiza mlimpa wenyewe kiburi kwa kumuita Mfalme wa Chura fc,sasa mnalalama kitu gani!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic