August 13, 2016





Kuna taarifa kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa limefungua tena dirisha la usajili kwa saa 48.

Taarifa kutoka ndani ya TFF zinasema Kuanzia leo, dirisha hilo la usajili litafungwa Jumapili saa 6 usiku, kwenda Jumatatu na hii ni nafasi kwa klabu ambazo hazikuwasilisha usajili kukamilisha.

Mabingwa wa Tanzania, Yanga pamoja na Coastal Union pia African Lyon zilikuwa kati ya timu za Ligi Kuu Bara na Daraja la Kwanza ambazo hazikuwa zimekamilisha usajili.

Hii inaweza kuwa nafasi ya klabu hizo kumalizana na suala hilo ili kutulia na kulenga maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu Bara, wiki ijayo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic