August 6, 2016


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema amesikia kuna mtu ametoa Sh milioni 100 kuisaidia klabu moja na kuonekana ni mtu mwema Tanzania nzima.

Hali ambayo inamshangaza kwa kuwa kusaidia kwa upande wa Yanga tena kwa gharama ya juu ni jambo la kawaida kabisa.

Manji amesema hayo wakati wa mkutano wa dhararu wa wanachama aliouitisha kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo.

Ingawa Manji hajataja jina, lakini mfanyabiashara Mohammed Dewji alitoa Sh milioni 100 kusaidia usajili wa Simba.


“Nasikia wanasema ndiye tajiri namba moja Tanzania, ametoa Sh milioni mia kuisaidia klabu,” alisema Manji na wanachama wakashangilia.

5 COMMENTS:

  1. sio tariji no 1 tz tu hata afrika kwa vijana na ni wa 24 afrika kwa ujumla

    ReplyDelete
  2. Nilifikiri jamaa kaitisha mkutano kuwaarifu wanayanga uwanja aliowaahidi, kumbe ni kwenda kuwatangazia zile zile pipi zake. Jamaa mjanja sana amejenga mamlaka ya kutegemewa na kunyenyekewa, ukikosoa tu unafukuzwa uanachama.

    ReplyDelete
  3. Nilifikiri jamaa kaitisha mkutano kuwaarifu wanayanga uwanja aliowaahidi, kumbe ni kwenda kuwatangazia zile zile pipi zake. Jamaa mjanja sana amejenga mamlaka ya kutegemewa na kunyenyekewa, ukikosoa tu unafukuzwa uanachama.

    ReplyDelete
  4. mwaka huu hatutaki kudanganywa tena.kwa misimu mitano mfululizo tunatambulishwa wachezaji wapya katika samba day lakini ligi ikimalizika nafasi ya tatu au ya nne na msimu unaofuata nusu ya wachezaji wapya waliotambulishwa wanaachwa kwa kushuka kiwango.Kat5ika miaka saba tuliyoadhimisha Simba day tangu 2009,Ni mara mbili tu simba ilisherekea simba day ikiwa na kombe

    ReplyDelete
  5. Mimi ni shabiki waa Yanga wa muda mrefu, nahitaji kaddi ya Yanga niwe mwanachama kabisa naipataje?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic