August 13, 2016


Beki mpya wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy, ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukamilisha haraka sakata linalomkabili ili ajue hatma yake kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Kessy hajaichezea Yanga mechi yoyote kutokana na kuwa na mgogoro wa kimkataba dhidi ya klabu yake ya zamani, Simba, hatua ambayo imesababisha akose leseni ya kuitumikia Yanga.

Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mazoezi ya mwishoni ya Yanga ya kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MO Bejaia itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii inatarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu kupania.

Kessy alisema kikubwa yeye anataka kucheza mechi hiyo ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam akiwa kama mchezaji halali wa Yanga.

Kessy alisema, hivi sasa yeye hataki kulumbana na kiongozi wa Simba, kikubwa anataka kuona kanuni na sheria zikitenda haki, hivyo ameiomba TFF kulimaliza kwa haraka suala hilo ili katika mechi hiyo awepo uwanjani.

Aliongeza kuwa, amechoka kufanya mazoezi pekee na timu, badala yake anataka kucheza mechi za mashindano ili kulinda kipaji chake alichotoka nacho Simba.

"Suala langu lipo TFF, lakini hadi hivi sasa sijajua hatma yangu na mimi kikubwa ninataka nicheze mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam baada ya kuzikosa mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.

"Hivyo, ninaliomba shirikisho kumaliza suala kwa haraka ili mechi hiyo niwepo uwanjani, ninaamini suala litakamalika kabla ya kufikia Jumatano siku ya mechi.

"Nilikuwa sitaki kabisa kulizungumzia hilo suala kwa hivi sasa, nimefikia hatua ya kuliongelea hilo hivi sasa, baada ya kuona siku zinazidi kwenda na mimi ninahitaji kucheza,” alisema Kessy.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic