August 19, 2016


Bosi wa benchi la ufundi la Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amesema msimu wa 2016/17 ni mwendo wa Hapa Kazi Tu, hiyo ni kufuatia kumtimua kazini aliyekuwa msaidizi wake, Habibu Kondo kwa kile alichosema anataka watu wanaoendana na kasi yake.

Suala la viongozi kutumbuliwa kutokana na uvivu au kutokuwa sahihi, limekuwa maarufu sana kutokana na Rais John Magufuli kuanzia mfumo huo.

Julio amesisitiza kauli yake ya kutaka ubingwa akisema ni msimu wa maajabu kama Leicester City na katika kutaka kutekeleza hilo, ameamua kupitisha panga kwenye benchi la ufundi baada ya kuanza na wachezaji kutoka 32 wa msimu uliokwisha mpaka 23 atakaokuwa nao safari hii.

Kondo amekiri kutokuwa na kikosi na kwamba viongozi wa Mwadui wamekuwa wakimuahidi kumpa mkataba, lakini Julio mwenyewe amelifungukia Championi Ijumaa, kuwa Kondo hana chake na tayari nafasi yake imezibwa na Khalid Adam.

“Niliamua tu kumuondoa na watu wengine ambao walikuwa hawaendani na sera yangu. Nimedhamiria msimu huu ni wa Kazi Tu kama mheshimiwa rais (John Magufuli) anavyosisitiza na mimi katika kutekeleza hilo nimeamua niwe na benchi la ufundi la kazi tu na kikosi kidogo msimu huu.

“Nafasi yake nimemkabidhi Khalid ambaye juzikati alipata leseni ya Daraja B na ana weledi kwenye kitengo cha ukipa, hivyo atanisaidia sana kuwafundisha makipa.

“Nimeamua kuwa na ‘staff’ ndogo yenye ari, kasi  ya kazi, siyo rundo la watu wa kupiga porojo,” alifunguka beki huyo wa zamani wa Simba.


Aliwataja miongoni mwa nyota aliowaongeza kuwa ni Salum Kanoni kutoka Kagera Sugar, Nassor Masoud ‘Chollo’ (Stand United), Joseph Kimwaga (Azam) Abdallah Seseme, Miraji Athumani (Toto Africans), Rashid Ismail (Simba), William Lucian ‘Gallas’ (Ndanda) na  kumrejesha Paul Nonga kutoka Yanga. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic