August 24, 2016

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijm, amefichua kilichofanywa na wachezaji wake mpaka ikafanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa, huku akisema kadi walizopewa Donald Ngoma na Thabani Kamusoko zilichangia.

Yanga ambayo jana Jumanne ilikamilisha ratiba yake ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kucheza dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, haikuwa na msimu mzuri kwenye michuano hiyo hali iliyowashusha morali ya mashabiki wake.
   

Kamusoko

Pluijm

Kabla ya mchezo wao wa jana, Yanga ilikuwa tayari imeshacheza mechi tano dhidi ya MO Bejaia, Medeama na TP Mazembe na kufungwa tatu, sare moja na kushinda moja, ikikusanya pointi nne.

“Ni lazima tulipaswa kupata ushindi kwenye mechi za nyumbani, pia tulifanya makosa mengi kwenye safu yetu ya ulinzi na hiyo ndiyo ilitufanya tufungwe mabao ambayo mengine ni ya kizembe.

“Kiukweli mechi za nyumbani ni lazima ushinde, usipofanya hivyo kwako unadhani utawezaje ugenini, yote kwa yote huu ni mpira, tunakubali matokeo ya aina yoyote yale.

Katika hatua nyingine, Pluijm alisema kitendo cha kuwakosa mara kwa mara wachezaji wake ambao wengi walikuwa ni watovu wa nidhamu na kulazimika kukosa mechi kutokana na kutumikia kadi za njano na nyekundu kilichangia hali hiyo.

Ikumbukwe kuwa, katika mechi hizo zote mpaka Yanga inamaliza mchezo wake wa jana ambapo ilifungwa mabao 3-1 na TP Mazembe, iliwakosa Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Vincent Bossou na Kelvin Yondani, ambao walikuwa na kadi mbili za njano huku Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakikosa baadhi ya mechi kwa kuwa na kadi nyekundu.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic