August 28, 2016

Straika chipukizi Marcus Rashford, jana aliiwezesha Manchester United kupata ushindi baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa Premier League dhidi ya Hull City, ambapo aliingia akitokea benchi.

Pamoja na furaha aliyoipata kutokana na ushindi huo, Rashford ambaye ana umri wa miaka 18, ameambiwa na kocha wake, Jose Mourinho kuwa anatakiwa kuendelea kuonyesha ubora kwakeili apate nafasi na hiyo siyo uhakika kuwa atacheza katika mchezo ujao dhidi ya Manchester City.
  





Timu hizo zinatarajiwa kukutana Septemba 10, mwaka huu katika mechi inayojulikana kwa jina la Manchester Derby.

“Huwezi kumtoa mchezaji kisa tumefanya vizuri, mchezaji wetu chaguo la kwanza katika ushambuliaji ni (Zlatan Ibrahimovic) mchezaji mwenye uwezo wa juu. Siyo kwamba ni mfuungaji tu lakini anaonyesha ushirikiano na wenzake na wanacheza vizuri.

“Rashford anaweza kucheza au anaweza kuanzia benchi, kijana huyo atacheza mechi nyingi msimu hu, najua alionyesha uwezo mzuri msimu uliopita na sasa nafanya naye kazi, namjua vizuri,” alisema Mourinho.

Rashford pia alifunga bao katika mechi dhidi ya Leicester City katika Ngao ya Jamii wiki mbili zilizopita.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic