August 5, 2016



Nahodha wa Simba, Mussa Mgosi amefunguka kuwa, klabu yao inapoelekea kusherehekea kutimiza miaka 80, hiyo ni ishara tosha kwamba inazaliwa upya, hivyo wapinzani wao wakae mkao wa kuumia kila msimu.

Jumatatu ijayo Simba inatarajiwa kusherehekea kutimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake ambapo sherehe hizo zitafanyika kwenye Tamasha la Simba Day ambapo kikosi hicho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya FC Leopards ya Kenya.

Simba ipo kwenye maandalizi kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 20, mwaka huu, ambapo kwenye maandalizi yao ilipiga kambi mkoani Morogoro na kucheza mechi nne za kirafiki na jana Alhamisi kikosi hicho kilitarajiwa kurejea jijini Dar.

“Kambi tumemaliza salama na naamini mwalimu amekiona kikosi chake kimeiva. Nisema tu huu mchezo wa mwisho ambao tumefungwa bao 1-0 dhidi ya KMC ni kipimo tosha kwetu kwani zile mechi za awali tulikuwa kama tunawaonea, walikuwa hawatoi upinzani wa kweli na hawa jamaa kweli wametupima na tumeona wapi kuna upungufu.


“Niwaombe mashabiki wa Simba wakae mkao wa kupokea mataji kwani Jumatatu ijayo klabu yetu hii inazaliwa upya, hivyo baada ya hapo timu nayo itakuwa mpya na tutaanza kuchukua mataji moja baada ya lingine,” alisema Mgosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic