August 22, 2016

Kocha wa New York City FC, Patrick Vieira ambaye ni kiungo wa zamani wa Arsenal na Inter Milan amempa ushauri Mfaransa mwenzake, Paul Pogba kuwa anatakiwa kuonyesha uwezo kuthitisha thamani yake na kutotaka kufanya yake yanayofanywa na mastaa wengine wa dunia.

Pogba ambaye ana umri wa miaka 23 anatajwa kuwa ndiye atakuwa Vieira mpya katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa, amesajiliwa Manchester United hivi karibuni kwa dau la pauni milioni 89, ada ambayo imemfanya kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kununuliwa katika soka duniani.


  “Mimi ni shabiki mkubwa wa Pogba, nafikiri ni mchezaji wa kiwango cha juu, hilo halina ubishi, atakutana na presha kubwa ambayo yote atatakiwa kuibeba yeye na kuidhibiti.





“Kama akiona atashinda mechi kwa kutegemea nguvu zake pekee hilo ni kosa kubwa, anatakiwa aitengeneze timu ili iwe inabalansi na siyo yeye kutumia nguvu kubwa, nimesoma sehemu kutoka kwa Mourinho kuwa atafanya mazuri na kuwa kama Messi au Ronaldo.



“Kama watu wanategemea mabao 40 katika msimu mmoja hilo siyo jukumu lake, asiwaige hao, yeye anatakiwa kuwa na utambulisho wake,” alisema Vieira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic