August 21, 2016




Na Saleh Ally, Barcelona
Niliingia kwenye Uwanja wa Camp Nou hapa jijini Barcelona, Hispania, jana na kushuhudia mechi ya kwanza ya FC Barcelona ambao ni mabingwa watetezi wa La Liga.

Mechi hiyo ya kwanza msimu huu, imekuwa nzuri kwao baada ya kuivurumisha Real Betis kwa mabao 6-2.

Nahodha Lionel Messi, alipiga mbili. Mshambuliaji hatari, Luis Suarez akapiga hat trick na ilikuwa mechi yenye ushindani kweli.

Nimejifunza mengi, lakini hili la akinadada warembo, nikaona ‘nishee’ nanyi. Ukiingia unakutana na akina dada warembo waliopendeza kwa kuvaa magauni ya rangi nyeusi na mikanda ya rangi nyekundu.

Kama umepotea, au una swali, basi kina dada ndiyo wamnafanya kazi hiyo kuhakikisha kila mmoja anafika sehemu sahihi.

Wanahakikishia kila mtu anaingia na kuondola salama baada ya mechi.

Tena wanavyokupokea ni kama mteja hasa, maana tabasamu la kutosha linaloashiria huduma bora.

Uwanja wa Taifa, ni walinzi tu. Tena kila mmoja kakunja sura, akitaka kuonyesha kila anayekwenda pale ndiye mwenye shida.

Ni kama Yanga, Simba au timu nyingine hazihitaji watu. Wanajipeleka wenyewe na wasipokwenda, shauri lao.

Barcelona inaonyesha nini maana ya huduma, inabembeleza wateja, inapambana kutoa huduma bora. Sasa itakuwa ni Yanga na Simba? Hapa nimeona kuna jambo la kujifunza.

Limeniamsha na kugundua kumbe watazamaji uwanjani, ni wateja. Hivyo tuachane na mawazo ya kuamini watu hupelekwa uwanja wa taifa na shida zao. Wahusika wawe wabunifu kidogo na tukubaliane, si kila mlinzi wa sehemu, lazima atumie nguvu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic